Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema uhai wa Chama Cha Mapinduzi ni wanachama walio hai hivyo, amewataka Viongozi wa CCM kuhakikisha Idadi ya wanachma wanaojiunga na CCM inazidi kuongezeka.
 
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wa Jimbo la Ziwani na Jimbo la Wawi ambapo amesema ni vyema kuwa na takwimu sahihi za Wanachama ambazo zitatumika kupata Idadi sahihi ya wapiga Kura ambao watakivusha Chama ifikapo mwaka 2025
Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Ilani ya CCM inaendelea kutekeleza Ilani kwa kujenga miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo, amewataka Wananchi kutoe mashirikiano kwa Serikali ili kuweza kukamilisha miradi hiyo.
Aidha amewapongeza Wananchi wa Ndagoni waliotoa maeneo yao ya kilimo kwa kupisha Mradi wa ujenzi wa Barabara maamuzi ambayo yanaonesha utayari wa Wananchi kuungana na Serikali yao katika ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
Amewataka Wananchi kuendelea kuziunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt.  Hussen Ali Mwinyi na kuwahakikishia kuwa miradi yote iliyotajwa katika Ilani na ile iliyoelekezwa na Rais  inatekelezwa kwa faida ya wazanzibari.
 
Amefahamisha kuwa mkakati wa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongzwa na Dkt Hussen Ali Mwinyi ni kuhakikisha wanawawezesha Vijana na Wanawake kupitia miradi mbali mbali ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili nao waweze kunufaika na matunda ya CCM na Serikali kwa ujumla.       
 
Aidha amewataka Wananchi wa Majimbo hayo kuendelea kuishi kwa Amani na Upendo ambao ndio msingi wa maendeleo na kuwataka wapenda maendeleo kuiunga mkono CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka Viongozi wa CCM kwa Ngazi zote kuchangamkia fursa mbali mbali na kuzielekeza kwa Vijana wanaojitolea katika Chama ili kujipatia kipato na kupungua ukali wa maisha.
 
Nae Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chakechake Ndg. Ali Muhamed Chande ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kulinda Amani na utulivu uliopo hatua ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa kuweza kufikia maendeleo iliyojipangia.
 
Amewataka wananchi kuendelea kuungana na Serikali katika kuilinda Amani na utulivu ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa shughuli mbali mbali za kijamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mhe. Dkt. Abdallah Rashid ameeleza kuwa Serikali kupitia dhana ya uchumi wa buluu imejenga kiwanda cha kuanikia Dagaa eneo la Ndagoni hatua ambayo itawasadia waanika dagaa kuweza kufanya shughuli zao bila ya changamoto zozote.
Katika ziara hiyo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amepokea Taarifa za utekelezaji wa Majimbo hayo na kukagua ujenzi wa Matawi na Maskani kwa lengo la kuimarisha Chama na Jumuiya zake.
 
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

0 comments:

 
Top