Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan amewataka Madaktari wa Hospital ya Wilaya ya kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja kuendelea kutoa huduma bora ili kusaidia kuimarisha Afya za wananchi.
Mama Sharifa ametoa wito huo alipofika kuwajuulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo pamoja na kuwapa zawadi za Eid akiambatana na viongozi mbali mbali.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi Imedhamiria kuboresha huduma za Afya ili wananchi wake wapate huduma bora.
Mama Sharifa ameeleza kuwa lengo la kufanya ziara hiyo ni kuwafariji na kuungana nao katika kipindi hichi cha Eid El Fitri jambo ambalo linazidisha umoja , Mshikamano na mapenzi baina ya wazanzibari.
Sambamba na hayo Mama Sharifa ametumia fursa hiyo kuwapongeza Madaktari wa Hospital ya Wilaya ya Kivunge kwa kujitolea kuwahudumia wagonjwa hatua ambayo inaongeza Imani ya Serikali kwa watumishi wa kada ya Afya.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Muhamed Mahmoud amemshukuru Mke wa Makamu wa Pili wa Rais kwa kuamua kuwatemebelea wagonjwa katika Hospital hiyo na kueleza kuwa ziara hiyo ni ya Kwanza kufanyika katika Mkoa huo.
Aidha Mhe. Ayoub ameeleza kuwa changamoto ya upatikanaji wa Dawa za Ganzi kwa wagonjwa wa Maradhi ya Kisukari atalisimamia ziweze kupatikana kwa wakati na za kutosha.
Katika Ziara hiyo Mama Sharifa Omar Khalfan amefuata na viongozi mbali mbali akiwemo Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Bi Khadija Shamte ambapo ameeleza kuwa Tume ina mkakati wa kuanzisha Sheria ya Bohari ambayo itasaidia wananchi kuweza kupata huduma ya Dawa kwa urahisi zaidi.
Abdulrahim Khamis
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment