Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 zilizomo katika bara la Afrika na ni moja wapo nya nchi 7 za Umoja wa Afrika Mashariki.
Kabla ya mwaka 1964 hakukuwa na taifa liitwalo TANZANIA. Kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, ambapo mara baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na kulifaya kuwa taifa huru ambalo liliweza kujiendesha wenyewe bila ya kusimamiwa na mtu mwengine kutoka nje ya Afrika.
Baada ya uhuru wa Tangayika ambao ulikuwa 1961, nayo Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka kwa Muingerea mwaka 1963 ambapo uhuru huu ulidumu kwa siku chache tu ambapo mwaka 1964 serikali iliyopata uhuru mwaka 1963 ilipinuduliwa mwaka 1964 na hapoa kukaifanya Zanzibar kuwa huru mara mbili, ule wa Muengereza na Sultan.
Uhuru wa mataifa haya mawili ndio uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aprili 26, 1964, makuliano ya viongozi wawili wakuu wanchi kwa wakati huu Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndio chanzo kikuu cha kuwepo Tanzania ya leo.
Makubalino ya kuwepo kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yalitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume na aliyekuwa Rais wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere visiwani Zanzibar 1964.
Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo yaliweza kuthibitishwa na Bunge la Tanganyika pamoja na Baraza la Mapinduzi tarehe 26 Aprili, 1964. Ambapo Tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam na kubadilishana hati za Muungano, ambapo pia sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ibara ya 4 kwamba:
“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano). Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Aidha, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania una vyombo viwili vikuu venye mamlaka sawa ya kiutendaji ambavyo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ambayo ndio serikali kuu na ya pili ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mbali na hayo, kuna vyombo viwili vyenye mamlaka na kutekelezaji wa utoaji wa haki kwa wananchi ambapo kuna Mahkama Kuu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na pia kuna Mahkama kuu ya Zanzibar. Mbali na hayo ndani ya Muungano pia kuna na vyombo viwili yya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za ummah ambavyo ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, ambapo hii ni taasisia mbili tofauti ambazo zinaweza kutegemea na kubadilisha taarifa muhimu pale inapohitajika kufanya hivyo.
Kwa kuwa tumo ndani ya muungano ya nchi mbili tofauti katika mgawanyo wa kazi na utendaji wake, hivyo basi ipo haja kwa jamii na hasa kwa kizazi kipya kufahamu kwamba kuna baadhi ya mambo ya kiutendaji yapo chini ya usimamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa yanayohusu mambo ya Muungano kama ambayo yamebainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Aidha, yapo baadhi ya mambo yanaendeshwa na kutekelezwa moja kwa moja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hasa yale yote ambapo yapo nje ya makubali au hati ya muungano.
Wasimulizi kuhusu kuwepo kwa Muungano huu ni wengi na kila mmoja na sababu zake, wapo waliingia kwenye siasa za TANU na ASP, wapo wanasilimu sababu za kiisimu kama vile lugha, ukaribu wa baana ya watu wa Zanzibar na Tanganyika, lakini pia wapo wanaosimulia kuhusu suala zima la biashara katika ya Zanzibar, Tanganyika na nchi yengine za jirani ambazo Zanzibar ilikuwa ikifuta biaadha katika mataifa hayo kama vile Kongo, Malawi n.k.
Aidha wapo pia wanaosimulia kwamba sababu kuu Zanzibar kuunga na Tanganyika ni kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama mara baada ya kufanyika mapinduzi ya Zanzibar hali ilionikena kama bado haijatengemaa hivyo wazo la kuziunganisha nchini lilionekana ni la muhumu sana kwa ustawi wa Zanzibar .
Hatuwezi kukataa au kupinga kwa kuwepo kwa sababu nyengie mbali mbali kwa mujibu wa historia, lakini bado tunaweza kusema muungano unaweza kuwafanya baadhi ya watu kujuwa asili zao kutokana na historian na mienendo ya koo zao za awali ambazo zilifika Zanzibar kabla ya uhuru wa 1963 na mapinduzi ya 1964.
Kwa sasa tayari Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetimiza miaka 58, ambapo yapo mambo mengi yanahitajika kujulikana na hasa kizazi hiki cha sayansi ya teknologia, ingawaje faida zipo nyingi za muungano lakini pia na matito yapo mingi ya muungano, kwa mfano:- wanasiasa wengie wamekuwa wakipika kelele kuhusu hati ya muungano naaminni baadhi yao hawakuwepo katika wakati huo wa miaka 58 iliyopota.
Maneno kama haya wanasiasa yanaweza yakawa hayana faida lakini yana mantiki kwa kizazi cha sasa. Ingawaje uwepo wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni miongoni kwa kielelezo tosha cha uwepo wa Hati ya Muungano.
Aidha, inasemekena Hati za Muungano zilitiwa saini na waasisi wa Muungano tarehe 22 Aprili, 1964 visiwani Zanzibar ambapo ndio iliyopelekea kufuta jina la Tanganyika na kulibakisha la Zanzibar, ikumbukwe kwamba kwa upande wa Tanganyika walitoa herufi tatu ambazo ni TAN ana kwa upande wa Zanzibar nao walio hizi hizo hereufi tatu ambazo ni ZAN na baadae kuwekwa sawa kwa kujaziwa heribu na kuwa TANZAN (ia) na sasa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika makubaliano hayo katika ya Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni kwamba Mwalimu Nyerere atakuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya ya Muungano wa Tanzania na Sheikh Karume atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo ndivyo ilivyokuwa lakini kidogo kidogo tulianza kubeza makubaliano hayo na hatime kubadilishwa na sasa Rais wa Zanzibar amekuwa kama Waziri badala ya Makano wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sio jambo baya ila limekengeuka makubalino ya awali ambapo wahenga walisema asiyekuwepo na lake halipo.
Mabadiliko hayo ya kumuondosha Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Jamuhuri pia ni miongoni mwa malalamiko wa wananchi wa Zanzibar kwani inaonakana kumuondosha Rais wa Zanzibar katika nafasi ya Umakamo ipo kisiasa zaidi kuliko kufuta makubalino ya hati za Muungano ya mwaka 1977.
Hata hivyo, Aprili 26, 1964 Bunge la Tanganyika lilipitisha Sheria za Muungano, ambapo Sheria hizo pia zilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar. Sheria hizo za Muungano zilithibitisha kuwa ndio hati za Muungano, ambapo zilimtaja Rais na Makamu wa Rais pamoja na mufumo au muundo wa Muungano na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Aprili 27, 1964, waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni Sheikh Abeid Amani Karume, Kassim Abdala Hanga, Abdulrahaman Mohamed Babu, Hassan Nassor Moyo, Sheikh Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Sheikh Idris Abdul Wakil. Baada ya kuapishwa kuwa Wabunge wakateuliwa kuwa Mawaziri wa Serikali ya Muungano.
Kabla ya Muungano, kulikuwa na Katiba ya Tanganyika ya mwaka 1962 na upande wa Zanzibar kulikuwa na Amri za Katiba (Decrees). Katiba ya Tanganyika baada ya kufanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya Muungano iliendelea kutumika kama Katiba ya Muungano ya mpito hadi mwaka 1977 ilipopitishwa Katiba ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria za Muungano.
Aidha, katika marekebisho hayo yalimtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais, akiwa ni msaidizi wa Rais kwa masuala yote ya kiutawala kwa upande wa Zanzibar, na Waziri Mkuu kuwa ni Makamu wa Pili wa Rais ambaye atamsaidia Rais kwa masuala yahusuyo upande wa Tanganyika na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliainisha mambo kumi na moja ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano chini ya usimamizi wa Serikali ya Muungano ambayo ni pamoja na Katiba na Serikali ya Muungano Mambo hayo ni: - Mambo ya Nchi za Nje; Ulinzi; Polisi; Mamlaka juu ya mambo yanohusika na hali ya hatari; Uraia; Uhamiaji; Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje na Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Mambo mengine ni Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha; na Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
Kuongezeka kwa Orodha ya Mambo ya Muungano yaliongezwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwa kushirikisha pande zote mbili za Muungano. Juni 10, 1965, mambo yote yahusuyo sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yoyote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusu fedha za kigeni yaliingizwa kuwa jambo la 12 la Muungano.
Lengo kubwa la kuongezwa kwa jambo hilo ilikuwa ni kuwa na sarafu ya pamoja ya Tanzania baada ya Muungano, na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na mabenki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki mwaka 1964.
Mwaka 1968, suala la maliasili ya mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa na gesi asilia liliongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano kuwa Jambo la 15.
Vilevile, kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 na kutungwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, mambo yafuatayo yaliongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano ambayo ni Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yanayohusika na kazi za Baraza hilo (Jambo la 16); Usafiri; Usafirishaji wa Anga (Jambo la 17) na Utafiti (Jambo la 18); Utabiri wa Hali ya Hewa (Jambo la 19); na Takwimu (Jambo la 20).
Kutokana na kuvunjika kwa Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki mwaka 1979, suala la Mahakama ya Rufani ya Tanzania nalo liliongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano na kuwa Jambo la 21. Vilevile, kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Nyalali iliyokusanya maoni ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Uandikishaji wa Vyama vya Siasa na mambo mengine yanayohusiana nayo liliongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano (Jambo la 22).
Suala hilo hatimaye lilipitishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura Namba 258. Utaratibu uliotumika katika kuongeza idadi ya mambo ya Muungano kutoka 11 hadi kufikia 22 ni kupitia maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muungano umechukuwa nafasi kubwa katika kuwaunganisha wananchi na kuimarisha mahusiano kati ya Bara na Visiwani.
Licha ya kuweongeza kwa mambo ya mungano na kutimia 22 ipo haya kwa taasisia husikiweka kuweka bayana baadhi ya mambo kama vile mambo ya muungano na kero za muungano au wizara za mungano na za SMZ hii itaweza kupungunza malalamika kwa jamii na kuliweka taifa katika hali njema kiafya na kiuchumi.
Aidha, ipo haja kufikiria au kuna kama ipo haja kwa baadhi ya mambo ya mungano kupunguzwa na kuyafanayia marekebisho baadhi, licha ya kwamba wananchini wamezoweza kusikia kwamba kwa sasa zipo kero kadhaa za muungano zimeondolewa lakini unapoangalia katiba ya Jamuhuri unaweza unakaona kama kuna mchozo wakuigiza tu.
Kero kubwa ya
muungano kwa sasa ni kwa wafanya biashara kulipia kodi zaidi ya moja hasa kwa
upande wa Zanzibar kwa sababu kuna Boti ya Mapato ya Zanzibar na Ile ya
Muungano, au pia suala la elimu ya juu hayo yote yanatakiwa kufanyiwa uhakiki
upya.
0 comments:
Post a Comment