Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na waumini wa Mskiti wa Mfereji wa Wima katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Akitoa Khutba Mskitini hapo Sheikh Muhammed Kassim amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuzingatia misingi ya kisheria katika Suala la uwalii katika Ndoa ili kuepuka zinaa kwa kutosihi ndoa hizo.

Amesema umefika wakati jamii ya wazanzibari wanadharau suala hilo na kuwataka kusoma Sheria ya Ndoa kabla ya kuozesha binti zao ili kuweza kuijua Sheria na kuifuata.

Akitoa salamu zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka waumini kujihimu katika kulea mayatima ili kuwaongoza katika malezi mazuri na yenye Maadili.

Akigusia maendeleo yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Nane Mhe. Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar kuacha habari za kupotosha kuhusu miradi inayoendelea kujengwa na kueleza kuwa azma ya Rais Dkt Mwinyi ni kuweza kuijenga Zanzibar kimaendeleo.

 Mhe. Hemed amesema fedha zinazotumika katika miradi hiyo ni za wananchi na kuwataka kutoa taarifa sehemu husika wanapoona ubadhirifu katika miradi hiyo

Amesema ahadi alizozitoa Rais Dr Mwinyi zinaanza kuetekelezwa kwa vitendo kwa miradi hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi wote


Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top