Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza Ushirikiano na uhusiano wake na Msumbiji katika adhma ya kuwajengea mustkbali mzuri wananchi wa pande zote mbili.
Mhe. Hemed alieleza hayo Ofisini kwake Vuga alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar.
Alisema, kuna kila sababu ya kuendeleza ushusiano kati ya Zanzibar na Msumbiji uliodumu kwa muda mrefu sasa kutokana na muingiliano wa watu unaosababishwa na harakati mbali mbali za kimaisha ikiwemo Biashara.
Makamu wa Pili wa Rais alieleza kuwa, wapo wazanzibar wengi wanaoendesha maisha yao Nchini Msumbiji kutokana na ushirikiano mwema uliojengwa miaka mingi iliopitwa.
Mhe. Hemed alimueleza Balozi AGOSTINO ABACAR TRINTA kuwa Zanzibar kuna fursa nyingi zinazopatikana akitolea mfano sekta ya utalii na bidhaa zitokanazo na masuala viungo (Spices).
Nae, Balozi mdogo wa msumbiji anaefanya kazi zake Zanzibar AGOSTINO ABACAR TRINTA Alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Nchi ya Msumbiji itaendelea kushirikiana na kufanya kazi zake kwa karibu na serikali ya mapinduzi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa lengo la kuimarisha Diplomasia.
Kassim Abdi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment