Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serekali anayoiongoza  itaendelea kuthamini  mchango mzuri  unaotolewa na vyama vya ushirika katika kuimarisha hali za maisha ya wananchi  kiuchumi na kijamii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed  alieleza hayo katika Hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Mwinyi  katika Maadhimisho ya siku ya kimataifa  ya ushirika Duniani  iliofanyika katika ukumbi wa sheikh Idriss Abdulwakili  kikwajun  jijini  Zanzibar.

Alieleza kuwa, Serekali imedhamiria kuingia katika uchumi wa Bluu kwa lengo la kutumia rasilimali za bahari ili kuleta Mapinduzi ya kiuchumi  ambapo vyama vya ushirika vina jukumu kubwa  la kushirikisha makundi yote yalimo katika jamii ili kufikia lengo hilo la Serekali lillilokusudiwa.

Makamu wa Pili wa Rais alisema jamii ina paswa kufahamu kwamba mbali na maeneo makuu ya uchumi  wa Buluu ambayo ni machimbo ya mafuta na gesi,ujenzi wa viwanda vya uvuvi ,usafirishaji na utalii dhana ambayo imepanga kushirikisha makundi yote katika jamii ikiwemo makundi ya vijana,watu wenye mahitaji maalum,wanawake na wazee.

Alisisitiza kuwa,vyama vya ushirika vina wajibu wa kuendeleza uzalishaji wa mazao ya Ardhini yakiwemo,mbogamboga,matunda,maziwa,nafaka,mazao ya mizizi na mengineyo ili kuwalisha wananchi na wawekezaji watakao kuja kuekeza katika shughuli za uchumi wa Buluu.

“Ustawi wa vyama hivi haujafikia kiwango  vya kuridhisha vikilinganishwa na vyama vya wenzetu nchi jirani,tunataka kuona vyama vipo imara ,kimuundo na uendeshaji” Alisema Mhe.Hemed .

Mhe. Hemed alisema Zanzibar imedhamiria kuimarisha matumizi ya teknoloji za habari katika uendeshaji  wa shughuli za kiuchumi  ambapo vyama hivyo vitasaidia kuleta msukumo  wa jamii kutumia teknolijia hizo.

Alifafanua kuwa, matumizi hayo ya Teknolojia  yatasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kutoa faida nyingi za kiuchumi zinazopatikana ikiwemo ununuzi wa Mazao ya jumla,kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa shindani katika soko la ndani  masoko ya kikanda (SADE na COMESA) hadi kufikia masoko ya kimataifa.

Akigusia faida zitokanazo na ushirika Makamu wa Pili wa Rais alisema vyama vya ushirika ni taasisi muhimu za hiari zenye uwezo  wa kutatua changamoto za kimaisha,kiuchumii  na kijamii kwa wananchi wake na kuleta ustawi wa maisha yenye neema kwa jamii.

“Hivi sasa vyama hivi vinatoa fursa kwa wanachama  wake kujiajiri  na kuajiri wengine ,vina uwezo mkubwa wa kuongeza uzalishaji mali na bidhaa mbalimbali” Alieleza Makamu wa Pili.

Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Pili wa Rais ameutaka uongozi wa Wizara ya Nchi Afisi ya Rais kuwajengea  uwezo,kuvikagua na kuvisimamia vyama vya ushirika  kwa lengo la kutoa haki  na kuondosha manungu’niko  ya wanachama.

Aliukumbusha uongozi wa Wizara hiyo kwamba  wakati umefika sasa wa kuviunganisha vyama vya ushirika Zanzibar katika mashirikiano ya Kimataifa yanayohusiana na masuala ya ushirika kutokana na fursa nyingi za kielimu sambamba na kubadilishana uzoefu ,matumizi ya Teknolojia ,mbinu za usimamizi,ubunifu na mtandao wa masoko.

“Katika hatua za kuimarisha vyama ushirika inatulazimu kuhimiza  matumizi ya Teknolojia  ya Habari (TEHAMA)katika uendeshaji wao,kufanya hivyo itasaidia kupata Tarifa sahihi  na za uhakika kujifunza  kutoka kwa wengine  na kudhibiti mapato ya wanachama” Alisema Makamu wa Pili wa Rais

Akisoma risala kwa niaba ya wanaushirika Katibu wa Muungano wa Vyama vya Ushirka  (CUZA) Bw. Suleiman Mbarouk Ame alimuahidi Mhe. Rais Dk. Mwinyi kuwa umoja wa wanaushirika utaendeleza jitihada kupitia sekta mbali mbali ikiwemo kushiriki katika masuala ya kilimo cha baharini nan chi kavu.

Alisema wanaushirika wanampongeza kwa dhati Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uzalendo wake wa kuviinua vyama vya ushirika na kuamua kuviweka chini ya Ofisi yake jambo ambalo linaashiria dhamira njema alionayo juu ya Wanaushirika wote wa Zanzibar.

Bw. Suleiman alieleza kwamba miongoni mwa mafanikio walioyapata  vyama vya SACCOS  vimefanya kazi kubwa ya kujenga mtaji unaofikia Shillingi Billioni 18.2 hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu  kupitia michango ya kuweka akiba na Amana za wanachama kupitia SACCOS 216 za Unguja na Pemba  fedha ambazo zinatatua changamoto za mtaji kwa wanachama wake.

Akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Afisi ya Rais kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhani Soraga alisema vyama vya ushirika ni taasisi muhimu za kiuchumi ambapo zaidi 20% ya nguvu kazi imejiajiri au kuajiriwa kupitia sekta ya vyama vua ushirika .

Pia alimueleza Makamu wa Pili wa Rais vyama vya ushirika vinasaidia kuingizia serikali mapato kwa kulipa kodi, leseni na vibali mbali mbali ambavyo vinasaidia kukuza uchumi wa Nchi.

Aidha, Mhe. Soraga alisema vyama vya ushirika vina mchango mkubwa katika kukuza demokrasia, haki za binadamu, Usawa pamoja na kudumisha Amani ya Nchi. 

Mapema, Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed alitembelea Mabanda ya wajasiriamali katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakili kikwajuni na kuskiliza changamoto zinazowakabili wajasiriamali waliokuwepo katika vyama vya ushirika.

Ujumbe wa Mwaka huu unasema Kwa Pamoja Tujenge Ushirika.

Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

0 comments:

 
Top