Mashirikiano mema baina ya wananchi wa Zanzibar ni alama Muhimu ya kumuenzi aliyekuwa Makamu wa kwanza Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad na hivyo hapana budi kuyaendeleza.
Othman Masoud Othman ambaye ni Mjumbe wa kamati Kuu ya chama cha ACT wazalendo aliyaeleza hayo leo (jana) katika Ukumbi wa chama hicho huko Mtambile Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba
Alisema mashirikiano hayo yalionekana tangu enzi za uhai wake hadi kufariki kwake ambapo wazanzibari wote walionyesha hisia.
“Na sisi wanachama na viongozi kwa pamoja lazima tuyaendeleze yoote aliyotuachia mzee wetu wetu kwani kufanya hivyo ndio tumemuezi kwa vitendo” aliseleza Othman.
Alifahamisha kuwa kila alichokiasisi Maalim Seif kilikuwa kinasimama na kuwa muhimu kwa sababu alisimamia umoja na upendo.
Makamu huyo wa Kwanza pia aliwaambia wafuasi wa chama hicho kuwa chama chao kimekuwa nguzo muhimu katika siasa za Tanzania kwa sababu waliwekewa misingi ya umoja, upendo na ukweli miongoni mwa wananchma.
Alisema umoja wao huo katika ACT wazalendo ndio utakaowafanya kuingia katika Chaguzi mbali mbali na kuibuka washindi.
Mapema Mjumbe wa Baraza kuu la chama hicho Ismail Jussa Ladhu alisema kama wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla watakwenda kinyume na kuyasahau yale aliyoyaacha maalim Seif itakuwa wamefanyakosa kumbwa katika ulimwengu.
“Maalim alipenda sana umoja, upendo kwani aliaamini ndio njia pekee Zanzibar kuwa na wepesi katika kuwapatia maendeleo wananchi wake” alieleza Jussa.
Aliwataka wananchi hao wasikubali kugaiwa baina watu visiwa vya Unguja na Pemba.
“Asitokee mtu akatugawa baina yetu kwani Maalim mpaka anafika mwisho wa uhai wake katika ulimwenguu huu alikuwa anatuhimiza kuwa wamoja” alisema Jussa.
Maalim akikaribia mwisho wa maisha yake, alihimiza mashirikiano miongoni mwa wananchi hatua ambayo iliasisi kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo matunda yake yanaonekana katika jamii.
Kuwasili kwa kiongozi huyo kisiwani Pemba inaibua hisia mpya kwa wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kumfananisha na Aliyekuwa Mwenyekiti wao Marehemu Maalim Seif Sharif hamad ambaye alizoea kuwafikia wananchi katika vijiji mbali mbali.
Wananchi wengi Kisiwani Pemba wanamuelezea Othman kama Maalim Seif mpya katika medani kisiasa za Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Chama cha ACT wazalendo kimekamilisha ziara yake ya kumtambulisha kiongizo wao huyo kwa viongozi wa mikoa, majimbo na Matawi kwa upande wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment