Watoto Iternation Film Festival, ni tamasha la kwanza la watoto  nchini,  ambalo litazinduliwa rasmi tarehe 11/3/2021 na kumaliza tarehe 14/3/2021.

Tamasha hili  limejikita zaidi katika kuonyesha filamu maalumi za watoto ambo zipo kwenye rika la chini ya miaka 12.

Lengo kuu la tamasha letu ni kuwaweka pamoja watoto, kuwajengea uwezo na ufahamu wa mambo mbali mbali yahusuyo filamu ikiwa ni pamoja ya kutengeza filamu kwa kupitia mafunzo na semina ambazo WIFF imeziandaa.

Watoto Internationla Film Festival kwa kushirikiana na taasisi nyengine nchini imekusudia kufufua michezo ya kitoto ambayo kwa sasa imepotea na kupotea huko kunaleta shida katika kulinda na kuhifadhi mila, desturi na tamaduni za Zanzibar kwa kupitia watoto ambao ndio warithi wakuu wa tamaduni zetu na kizazi kijacho cha Zanzibar.

Katika tamasha la kwanza jumla ya filamu 32 zimepokelewa na filamu 30 ndio zitaonyweshwa.

Filamu hizo zimepokelewa kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo wenyeji Tanzania,Spain, Brasil, Ujerumani, Kolombia, Uholanzi, Ubeligiji, Ufaransa, Urusi, Bulgeria, Mexico na Argentina.

Lengo la tamasha ni kuwaweka watoto pamoja na kuweza kupaza sauti zao kupitia njia ya filamu ambapo WIFF tunaamini hii ni njia mbadala kwa watoto, kupaza sauti zao na kusilikzwa kwa vile jamii inakosa kuwasikiliza watoto na hivyo watoto kujiona wametengwa na jamii zao na hata pale wanapopata majangwa ya udhalilishaji pia kusikiliza ni hashida na wakati mwengine pia huadhibiwa.

Mbali ya kuwakusanya na kuwaweka pamoja watoto, lakini tunapenda kuwahakikishia wananchi kwamba kwa muda wote wa tamasha hapa Mapinduzi Square, kutakuwa na ulinzi na uslama wa hali ya juu kwa ajili ya kuwalinda na kuwahifadhi watoto wetu.

Licha ya ulinzi huo, ni vyema kwa kila mtu, mzazi, mlezi pindi wanapokuja kwenye tamasha letu nao wawe na hadhari kubwa juu ya usalama wa watoto na mali zao, kwani ni wajbu wa kila mlezi au mzazi kumlinda na kumchunga mwanawe, na pale kunapotokea khitifau basi Uongozi wa Watoto International Film Festival (WIFF) watashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua zaidi.

 Mbali na hayo, kupitia tamasha hili, itakuwa ni chachu muhimu ya kuweza kuwaweka na kuwakusanya pamopa watoto wote wenye ulemavu, kama vile wasio sikia, wenye shida ya kusema, walemavu wa viungo pamoja na watoto wenye Ualbino.

Aidha, mingoni mwa malengo yake makuu ni kuwawezesha watoto kuweza kufahamu haki zao za msingi, kwa mujibu wa sheria pamoja na wajibu wao kama taifa na viongozi wa kesho. Ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji vyao na kiviendelea kupitia tathia ya filamu nchini.

Tamasha la Watoto International film Festival, ni tamasha la pili la filamu kwa Zanzibar, lakini hili litakuwa ni maalumu na la kipekee na hasa kwa vile limejikita moja kwa moja kwa watoto, na hadi sasa zipo takribani filamu 100 za watoto tulizozipoke kutoka mataifa mbali mbali, ndani ya tamsha hili kutakuwa na siku tatu maalumu ambazo zimepewa jina la SHULE FILAMU ni maalumu kwa ajili ya kuwanda toto tu.

Tamasha hili la Watoto limedhaminiwa na ZSSF, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale,Purelife, Mozeti Tours and Safari, ZIFF, ZATO, Isam Tours and Safari, Mambo Tv, na Uroja Carnival

 

Ali Othman

Afisa Habari.

Watoto Internation Film Festival.

0715 422061.


0 comments:

 
Top