Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezitaka taaisis binafsi na jumuiya mbali mbali Nchini kuendelea kuwasimamia na kuwasaidia watu wenye ulemavu ili wapate haki zao za msingi.

Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akizungumza na uongozi wa Jumuiya inayosimamia watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar (ZAPDD) uliofika afisini kwake vuga kwa ajili ya kubadilishana nae mawazo.

Alieleza kuwa anaunga mkono    jitahada zinazoendelea kufanywa na jumuiya hiyo tangu kuanzishwa kwake na amewashauri viongozi hao kuendelea kutoa taaluma ili jamii nayo iweze kushiriki kwa urahisi katika kuwapatia haki zao watu wenye ulemavu wa akili.

Alisema serikali ya awamu wa nane inapenda kuona taasis hizo zinazojitegemea zinazotoa mchango wao kwa serikali pamoja na jamii zikiwa zimejipambanua kwa kutanguliza maslahi ya watu wenye ulemavu kwa kuaanda mpango kazi utakaoishawishi jamii kutoa michango yao moja kwa moja bila ya kuwa na shaka ndani yake.

Makamu wa pili wa Rais aliwaeleza viongozi hao kuwa zipo baadhi ya jumuiya utendedaji kazi wake sio wa kuridhisha kwani zimekua zikifanya kazi zake bila ya kuzingatia uwazi na uwadilifu kwa kutoweka mchanganuo wa kazi wanazozifanya jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada za kuwasaidia walengwa katika sekta mbal mbali ikiwemo Afya na Elimu.

Kwa upande wake Makamu mwekiti wa Bodi ya wadhamini ya watu wenye ulemavu wa akili Bw. Tamim Haji Said alimueleza Makamu wa pili wa Rais kwamba lengo la Jumuiya yao imejikita katika kutete na kushawishi juu ya upatikanaji wa haki za watu wenye ulemavu wa akili kwa maeneo tofauti.

Alisema, viongozi kwa kushirikiana na serikali wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa akili wanapata haki ya elimu kwa kusimia na kuratibu uanzishwaji wa Elimu Jumuishi Zanzibar jambo ambalo limezaa matunda hadi sasa mpango huo unaendelezwa na serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Bw. Tamim Alifafanua kuwa katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa akili wanapata huduma stahiki jumiya imetoa mafunzo ya kuwajenge uwezo watendaji wa taasisi mbali ikiwemo Mahkama, Polisi na watendaji wa Ofisi ya mwanasheria mkuu hali ilisaidia kupitishwa kwa sheria inayokubali ushahidi wa watu wenye ulemavu wa akili wakiwa mahakamani.

Pamoja na mafanikio hayo Makamu mwenyekeiti alimueleza Mhe. Hemedi baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa pamoja tatizo la kukosa Ofisi za kudumu hali inayopelekea pesa nyingi kupotea katika kulipia Kodi pamoja na changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa Fedha.

Aidha, Viongozi hao walimuomba Makamu wa Pili wa Rais kuangalia uwezekano wa serikali kuwasaidia kwa kuwapatia Ofisi sambamba na kuzisaidia familia zenye watu wa ulemavu wa akili ili kikmu mahitaji yao ya msingi.

Wakichangia katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi Mwanaidi Saleh Abdalla na mratibu wa Jumuiya hiyi Ahmad Kassim wamesema pamoja na changamoto ya udhalilishaji inayowakumba watu wenye ulemavu wa akili lakini bado wanaendelea kutoa taaluma kwa jamii jambo linalotoa mafanikio kutokana na wazazi wengi kuwa na muwamko wa kuwaandikisha watoto wao skuli.

Jumuiya ya watu wenye ulemavu wa akili imeanzishwa miaka ishirini (20) iliopita na ina jumla ya matawi sitini (60) Unguja na Pemba.

Mapema, Makamu wa pili wa Rais amefika katika makaazi ya Familia ya aliekuwa Makamu kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad  Mbweni nje kidogoi ya Jiji la Zanzibar kwa ajili ya  kuwapa pole na kuwafariji kufuatia kwa msiba wa kuondokewa na mpendwa wao.

Makamu wa Pili wa Rais ameitaka familia hiyo kuwa na subra katika kipindi hiki pamoja nakuendeleza umoja na mshikamo aliouwacha marehemu Maalim Seif na serikali itaendelea kushirikiana na familia hiyo wakati wote.

Makamu wa Pili wa Rais alifutana na mkewe Mama Sharifa Omar Khalfan pamoja na viongozi wa wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais sera, uratibu na baraza la wawkilishi.

Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

0 comments:

 
Top