Wanawake nchini wameshauriwa kuwachagua viongozi wenye kuwaletea maslahi katika masuala yao yanayowahusu ili kufikia malengo wanayoyakusudiwa. 

Mwenyekiti wa Vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na ujasiamali zanzibar  Siti Abass Ali ameleza hayo wakati akizungumza na vikundi vya Kinamama vya ujasiriamali katika nyakati tofauti huko Mwera batini  pamoja na Mtoni ikiwa ni muendelezo wa kuwakumbusha wanawake juu ya wajibu wao wa kuwachagua viongozi bora.

 

Amesema kitendo cha kuwapa dhamana ya utumishi  Wazalendo wenye muono wa kusimamia mambo ya msingi ya maendeleo ndio njia pekee itakayosaidia kupatikana kwa ufumbuzi  wa kusuluhisha matatizo mbali mbali  yanayowakabili. 

 

Bibi Siti alieleza kuwa  ni vyema kwa wanavikundi hao kuweka mkazo zaidi kwa kuwaangalia viongozi wenye kuweka kipaumbele  juu ya masuala ya wanawake ikiwemo kuwawezesha kiuchumi, kusimamia suala la amani na utulivu pamoja na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia. 

 

Aliwaomba akina Mama hao kuzingatia suala zima la  kuwadhibiti watoto na vijana  kwa lengo la kutokubali  kutumiwa na wanasiasa wakiofilisika kisera katika kuwaingiza kwenye vurugu za kuchafua Amani ya Nchi.

 

Wakichangia kikao hicho wanawake hao kutoka vikundu mbali mbali  wamemuomba Rais atakayepata ridha ya Wananchi walio wengi ajitahidi  kuyapatia ufumbuzi matatizo mbali mbali yanayowazunguuka Wananchi katika maeneo yao.

Wamesema miongoni mwa tatizo sugu linaowakabili ni pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama hasa katika kipindi hiki ambapo katika shehia ya Kibweni na Mwanyanya kumekuwa na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Aidha wananchi hao wameiomba mamlaka ya maji Zanzibar {ZAWA} Kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo iliyochukuwa muda mrefu huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma hiyo muhimu katika ustawi wao.

Kassim Salum Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top