Ni hivi karibuni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia mfuko wa jamii ZSSF, imeweza kukamisha ujenzi wa nyumba za kisasa takribani 210, ikiwa ni mwendelezo wa sera ya serikali Mapinduzi Zanzibar, kuwapatiwa makaazi bora na ya kisasa wananchi wake, kama ambavyo alifanya rais wa kwanza wa Zanzibar.

Kwa kuwa kila binaadamu ana haki ya kuishi na kuthaminiwa utu wake na jinsi yake, hivyo basi katika kukamisha ujenzi huo wa nyumba huko Mbweni, ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukusanya mapata ya taifa kwa ajili ya shughuli za  maendeleo ya taifa na watu wake kwa ujumla.

Ni vyema kwa serikali kupitia mfuko wa jamii, kusimamia miradi kama hii mikubwa, kwa ajili ya kumpunguzia mwananchi mzigo mzito wa ujenzi wa nyumba hasa ukingalia gharama za ujenzi zilivyo hivi sasa na kipindi cha miaka 20kilichopita.

Kwa kuwa Jamuhuri ya Tanzania kwa sasa ipo katika uchumi wa kati, hivyo ipo haja kupitia nyumba hizo za ZSSF iwe ni chachu ya kuendeleza uchumi na maaendeleo ya jamii kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Nd.Khamis Mussa, alieleza kwamba mradi wa nyumba hizo uligharimu jumla ya shilingi za Kitanzania bilioni 35, ambapo jumla ya majengo 10 yamekwisha kamilika.

Licha ya maelezo hayo, katibu pia alieleza katika mwezi wa Juni 2020, nyumba takribani 164, kati ya 210 zilikwisha uzwa kwa maana hiyo kati ya hizo zimebaki nyumba 46.

Kwa kuwa ni jambo jema, ipo haja wananchi kuipongeza ZSSF na serikali kuu, kwa hatua madhubuti iliyofikia katika kukamilisha ujenzi huo ambapo kila nyumba moja iliuzwa kwa mwananchi wa Tanzania.

Tunaipongeza serikali kwa kuweza kusimamia vyema na kuhakikisha kwamba Zanzibar nayo inakuwa kiuchumi na kufaidi matunda ya uchumi wa kati.

Inawezakana kabisa ZSSF kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar walisimamia vyema zoezi la kuuzwa kwa nyumba 164, ingawaje ingekuwa vyema kama vyumba hizi wamengeuziwa wafanyakazi ambao ndio wateja wakuu wa mfuko wa hifadhi Zanzibar.

Licha ya kuuzwa kwa wananchi, lakini pia ZSSF ingaweza kufikira kitu mbadala ambayo ni kuzikodisha kwa wafanyakazi wa mashirika na taasisi za ummah, kabla ya kuuza nyumba hizo ambazo kwa sasa zipo kwa wananchi ambao ni wazalendo, wa taifa hili.

Tunaposema kukodisha sio kama ZSSF wasiuze la khasha, wangeuza na wengeweza pia kukusanya  pesa za kuendeleza ujenzi mpya katika maeneo mengine, kwa mfano kama nyumba 164 zingekodishwa kwa wafanyakazi wa serikali ingweza kupunguza ujenzi holela, lakini pia uhakika wa kukusanya mapatao ya kila mwezi ungekuwepo, kwa sababu wanaokodishwa ni watendaji na makato ya kila mwezi yangefanyika kupitia mishahara yao kama ambavyo mataifa ya nje wanavyofanya na leo ndio tunawasifia kwamba wamefika hatua kubwa kimaendeleo.

Tunaposema nyumba zikodishwe sio kama hatupendi mfuko wa jamii usipate maendeleo au kuingia mipango yake ya ndani, la khasha, bali kukodisha ni nyenzo muhimu wa ukusanyaji wa kodi na kutunisha mfuko kwa ajili ya maendeleo zaidi.

0 comments:

 
Top