Kalamu za waandishi wa habari na vyombo vya habari, ambavyo kwa asilimia kubwa vimekuwa vikitumia lugha asili ya Kiswahili, vimeweza kuimarisha umoja uliopo sasa tangu mwaka 1964, lilipoasisiwa taifa la Tanzania.

Kwa upande wa Zanzibar Kiswahili kimegawika  katika lahaja tatu muhimu, mbazo ni Kitumbatu, Kimakunduchi na Kipemba. Uwepo wa lahaja hizo, haimanishi kwamba Kiswahili ndio kimepotea au kupotoka la khasha, bali ni ukuwaji na uimara wa lugha ya Kiswahili.

Na ndio maana  Baraza la habari Tanzania mwaka 2016 liliandaa KANUNI ZA MAADILI KWA WANATAALUMA WA HABARI kwa lengo la kuwatanabahisha wamiliki na waandishi wa habari umuhimu wao pamoja na kufuata maadili kama ambavyo imelezwa:- Machapisho yasipotoshe kwa makusudi au kuwaarifu isivyo wasomaji, watazamaji au wasikilizaji kwa kuweka au kuacha kitu kilichokusudiwa. Hakikisha hakuna vitu visivyo na msingi, vinavyopotosha au kukosa ukweli.

Na kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi katika ngazi mbali mbali mbali,  kama vile Udiwani, Uwakilishi, Ubunge pamoja na Urais ipo haja ya kusisitizana na kukumbushana kuhusu  matumizi sahihi ya lugha.

Kwa mfano unapowasikiliza viongozi wawili wa vyama vikuu vya upinzani kama vile CHADEMA au ACT Wazalendo, kwa kweli lugha zao hazioneshi kuwa na nia njema hata kidogo,  mbaya zaidi vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kueneza uchochezi na sasa unapoangalia ONLINE TV ambazo zipo kwenye Utube, sijuwi lengo nini?

Licha ya sheria na kanuni zilizopo kwenye taalumu ya habari, lakini kuna baadhi ya vyombo vya habari kwa makusudi vimekuwa vikienda kinyume na utaratibu huo, ingawaje mara nyingi lawama hupewa Mhariri pekee, wakati mwandishi naye anahusika kwa njia moja ama nyengine  katika huchangia katika matumizi mabaya ya lugha ya kiswahili.

Kutokana na matumizi mabaya ya lugha hivi karibuni tumeshuhudia vyombo viwili vya habari vikifungiwa na TCRA, ambavyo ni Clouds Tv pamoja na Wasafi Fm, mbali ya ukiukwaji wa sheria za habari, lakini vituo hivyo vilikuwa chanzo  kikubwa cha kubananga lugha katika baadhi ya vipindi vyao, hiyo ni mifano michache tu.

 

TCRA Kuvifungia vyombo vya habari, kutokakufanya kazi kwa muda, inawezekana ikawa ni jambo jema kwa mujibu wa mamlaka ya TCRA, lakini je kwa upande wa wagombe kutumia lucha zenye kuonyesha chuki na uchochezi tuseme tume ya uchaguzi haina mamlaka ya kuwaonya wagombea hao?.

 

Lakini pia ifahamike kwamba unapowatukana viongozi wa chama kingeni ndani ya wafuasi wako baadhi yao ni ndugu zao na ni watu wa muhimu sana kwako, je hamuoni kwamba matusi na zadharau zitawafanya baadhi ya wapia kura wenu kuwachukiwa na kuwakosesha kura na kuwapa mnao watukana?

 

Unaweza ukawa mwalimu mzuri sana lakini wanafunzi wako wakafeli sana kutokana na kutoka kutumia lugha nzuri au fasaha yenye kuwavutia na kukusikiliza pindi unaposomesha, hivyo basi ni lazima wagaomembe wawe na unapambanuzi wa mambo na kuweza kuwafahamu wapiga kuwa wao ni watu wa aina gani, hili litasaidia kufikishwa ujumbe lakini utumia wa maneno pia uangalie ni wapi pa kuyatumia na muda gani na kwa sabubu gani?

Aidha, lugha ya kiswahili ni tajiri na yenye maneno mengi matamu na  mazuri, ambayo yakitumiwa vizuri humvutia msikilizaji.

Kazi na jukumu kubwa la mwandishi wahabari ni kuhakikisha kwamba jamii inaishi kwa amani na sio jukumu lake katika kutukuza uovu, uhalifu au tabia zote mbaya katika jamii na  hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.

 Hivyo basi, uwepo na uhuru wa kila mtu kumili Online Tv nalo ni tatizo katika matumizi ya lugha, kwani ni dhahiri tv za kwenye mitandani hazina wahariri kila mtu hufanya atakalo na ndio maana asilimia kubwa za lugha za matusi kwa viongozi zipo kwenye tv hizo za mitandao, ni jambo la kusikitisha sana, kuona taaluma hii ya habari ambao ni nguzo muhimu katika mihili ya serikali ikiwa imekubwa na utata, utashi na uchochozi wa makusudi katika jamii.

 Ni vyema waandishi wasiandike au kuonyesha au kutoa maelezo zaidi ya uhalifu kwa namna yoyote ile, ambayo itaweza kushawishi au kuchochea watu kuiga au kufanya majaribio ya matukio hayo. Kama ambavyo baadhi ya video zinawerushwa kwenye makundi ya whatssap au kwenye Online zinakwenda kinyume na maadali.

 Inawezekana kabisa Online TV zikawa hazina wahariri au wapo ila hawana ujuzi wa kuhariri habari zao, kama wapo basi ni vyema wafahamu kuwa jukumu lao la kuhariri habari ni zito na la thamani sana kwao na taifa kwa ujumla.

 Hata hivyo, Wahariri hawana budi kujua na kuelewa mambo yaliyomo au kuonyeshwa katika habari, ili kutambua athari zake kwa wasomaji, watazamaji pamoja na wasikilizaji, ingawaje jukumu hili pia linapaswa kufanya na mwandishi mwenyewe kabla habari haijafika kwa mhariri.

 Ni wajibu wa vyombo vya habari kwa kupitia kalamu za waandishi wao, kufanya tathimini na uteuzi wa maneno katika kuwasilisha ujumbe wake, matumizi mazuri ya kiswahili,  yanapaswa yafanyike pia kwa viongozi wa  vyama vingine vya kisiasa, kwa ajili ya  kustawisha umoja na mshikamano ulipo nchini, si dhani kama yupo kiongozi ambaye anaweza kuyaongoza makaburi, walemavu na watu waliokata tamaa kutokana na madhila ambayo yanaweza yakasababisha na lugha zao au vyombo vya habari.

 Ni vyema tukafahamu kwamba, Habari au Tangazo lenye taarifa au ujumbe wenye kashfa, dharau, uchochezi au ushawishi wenye nia mbaya ni vyema isichapishwe, kwa maslahi ya ummah na jamii kwa ujumla.

 Kwa kuwa uchaguzi mkuu ni kielelezo tosha cha utawala bora, hivyo basi matumizi ya lugha jambo la msingi sana katika ustawi wa taifa huru  kwa ajili ya kudumisha Amani, mshikamano na maendeleo.

 Ni wajibu wa vyombo vya habari nchini  pamoja na taasisi husika kuchukuwa hatua madhubuti katika suala zima la usimamizi na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili, sio jambo la busara hata kidogo kwa kiongozi kutumia neno lenye kukirikhisha na hasa kwenye jukwaa kwa mfano ni aibu na fedha kiongozi kumwita kiongozi mwezio “mshenzi” hii sio lugha nzuri katika kuhubiri utawala bora na demokrasia nchini.

0 comments:

 
Top