Ikiwa tumebakisha siku chache kufika tarehe 28, kwa ajili ya kukamilisha kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu 2020, neon kukwabwa kwa sasa lilotawala katika vyombo vya habari, wananchi na wanasiasa ni Demokrasia.
Kwa
sasa neno demokrasi limekuwa kama nyimbo kila mtu anajuwa kilitamta na
kulitetea kwa mujibu ambapendavyo.
Maana
fupi ya neno hili demokrasi ni mfumo wa Serikali ambao watu huchaguzi viongozi
wanaowataka kuwaongoza kwa kuwapigia kura.
Kupiga
kura ni haki ya kila mwananchi kwa mujibu wa sheria kama ambvyo imeanishwa
katika katiba ya Jamuhuri ya mungano waTanzania na ile ya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ya mwaka 1983.
Na
kwa kuwa Mwandishi wa habari ni katika jamii, hivyo basi kwa mujibu wa katika
anayo haki ya kupiga kura, lakini pia anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya
uongozi kama ambavyo zimeanishwa katika sheria
Katika
uchaguzi wa mwaka 2015 kumi na nne
vilishiriki katika uchaguzi huo ambapo vya hivyo ni ACT-WAZALENDO, ADA-TADEA, ADC,AFP,CCM,CCK, CHAUMA, CUF, D-
MAKINI, DP , JAHAZI ASILIA, SAU, NRA, TLP na katika mwaka 2020 vimeshiriki vyama
kumi na saba ambapo katika orodha ya awali havikuwepo vyama vinne ambayo ni
UPDP,UMD,NLD na CHADEMA hao ndio walikosekana katika kinyanganyiro cha 2020.
Licha
ya wagombe hao wa viti vya urais kwa mujibu wa vyama vyao, kwa bahati mbaya
sana hakuna mwandishi wa habari aliyejitokeza katika kinyanganyiro hicho, licha
kwamba jamii inawaamini sana waandishi wa habari lakini hanakuna aliyejitokeza
ila wapo baadhi ambao wanategemea uteuzi kutoka kwa mteule.
Ingawaje
yapo matamko ambayo yanamtaka mwandishi yoyote atakaingia kwenye harakati za
kisiasa aachana na taaluma yeke ya habari na kuendelea na shughuli za kisiasa,
hii sio sahihi kwani itakuwa inamyima haki ya kushiriki katika harakati za
kimaendeleo katika taifa lake.
Ifahamika
kwamba uandishi wa habari ni taalumu
ambayo haiwezi kuwa mbali na siasa kwa vile ni maisha ya kila siku, inawezekana
kabisa mwandishi wa habari kupewa dhamana na kuitekeleza ipaswavyo.
Ubaya
ni pale mwandshi wa habari kuigeuza kalamu kuwa kisu na kuanza kuwakata wengine,
kwa nini tuifananishe kalamu na kisu ,
kwa sababu kalamu inatakiwa kuandika na kunakili kilicho chema kwa maslahi ya
taifa na jamii kwa jumla.
Wito
wangu kwa wandishi wa habari wawe makini na kuwa tayari kulitumika taifa katika
kuhakikisha kwamba hakuna mifarakano wala migogoro ambayo itapelekea taifa
kutokutawalika.
0 comments:
Post a Comment