Na Jumbe Ismailly - HANANG

SERIKALI imewatahadharisha baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminufu wanaotengeneza vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo,maarufu kwa jina la wamachinga kuwa haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanahujumu mapato ya serikali.

Akizungumza na wafanyabiashara katika Mji mdogo wa Katesh,wilayani Hanang,Mkuu wa wilaya ya Hanang,Ghaib Lingo alisisitiza kwamba ni vyema kila mmoja ajenge utamaduni wa kulipa kodi zake kihalali bila kutumia njia za ujanjaujanja.

Kwa mujibu wa Lingo endapo wafanyabiashara hao watakuwa waaminifu katika kulipa kodi za biashara zao wanazofanya,zitasaidia kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya,maji na miundombinu ya barabara.

“Kwa hiyo niwasihi ndugu zangu tuwe wazalendo kwa kumuheshimu Mungu kwa sababu serikali hizi zimnetoka kwa mungu kwa kulipa kodi zetu bila kutimiza ujanjaujanja,kwani mnapotimiza ujanja tukiwagundua serikali kutumia kidogo vyombo vyake mnaanza tena kupiga kelele,na mimi nisingependa kutumia sana vyombo labda ninyi mkinilazimisha.”alisisitiza Lingo.

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya alikiri pia kwamba vitambusho vinavyotumiwa na wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la wamachinga,vitaendelea kuboresha zaidi ili kuondoa changamoto zilizopo kwenye vitambulisho hivyo.

Aidha Lingo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Hanang alifafanua kuwa mauzo ghafi chini ya shilingi milioni 4 yanahitaji kuwa na vitambulisho ingawa vitambulisho hivyo bado wataendelea kuviboresha kutokana na kuwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na picha,majina huku wengine wakiazimana wanapokuwa wakifanya biashara zao.

“Na Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli alisema badi nitatoa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo na mtu akiwa na kitambulisho asibughudhiwe,naaba yake taasisi zinazokusanya kodi zingine zisimwingilie yeye tayari ameshalipa hiyo kodi.”alifafanua Mkuu wa wilaya huyo.

 “Kwa hiyo niwasihi ndugu zangu tuwe wazalendo kwa kumuheshimu Mungu kwa sababu serikali hizi zimnetoka kwa mungu kwa kulipa kodi zetu bila kutimiza ujanjaujanja,kwani mnapotimiza ujanja tukiwagundua serikali kutumia kidogo vyombo vyake mnaanza tena kupiga kelele,na mimi nisingependa kutumia sana vyombo labda ninyi mkinilazimisha.”alisisitiza Lingo.

Kwa upande wake,Rose Kamili ambaye ni mfanyabiashara na mkulima wa mazao pamoja na kumpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kuwaunganisha na kuwafanya wafanyabiashara hao waweze kufahamiana,lakini alilalamikia kukosekana kwa soko la zao la vitunguu,na hivyo kumuomba afike kata ya Basuto kuzungumza na wakulima wa zao hilo.

Kwa mujibu wa Rose ambaye kwa sasa ni mgombea wa udiwani wa kata ya Basuto alisema kwa bahati nzuri zao la vitunguu kwa sasa lina bei nzuri sana na ana uhakika kuwa Halmashauri ya wilaya ya Hanang itanufaika kwa kupata fedha za mapato yatakayotokana na zao hilo.

“Kwa bahati nzuri vitunguu vina bei nzuri sana na nina uhakika Halmashauri ya Hanang itafaidi sana kupata fedha za mapato kwa vitunguu hivyo kwa sababu gunia moja linaweza kwenda mpaka hadi shilingi 100,000/= hadi 200,000/=.”alisisitiza Rose.

Aidha wafanyabiashara hao pamoja na kuridhishwa na utaratibu ulioanzishwa na Mkuu wa wilaya huyo wa kukutana na makundi mbali mbali lakini pia walisema huyo ni mkuu wa wilaya wa kwanza tangu wilaya ya Hanang ilipoanzishwa na kuwashauri waunde umoja wa wafanyabiashara.

Hata hivyo Leodiger Cosmasi Asenga ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wadogo wadogo alitumia pia fursa hiyo kumuomba mkuu huyo wa wilaya anapotaka kukutana na wafanyabiashara hao apange ratiba ya mikutano ya mchana ili wawe wameshasambaza bidhaa zao kwa wateja wao.

0 comments:

 
Top