Kwa kawaida waandishi wanatakiwa wawe makini katika kazi zao badala ya kuwa wasaka tonge, kwani kuna maisha baada ya uchaguzi na ni muhimu kuangalia maslahi ya taifa na jamii yako. Wapo waheshima kila mara hunukuu kwa kusema “kalama ya mwandishi ni hatari kuliko bomu la atomic” lakini pia baadhi yao hudiriki kusema “endepo kalamu ya mwandishi wa habari itatumika vyema itasaidia katika ujenzi wa taifa na kinyume chake ni kuliangamiza taifa” na hili halitaki tochi kwani mifano ipo mingi hata katika baadhi ya nchi wanachama wa jumuia ya Afrika ya Mashariki. Inahudhunisha kwa baadhi ya wanasiasa, licha ya kwamba baadhi yao, wameupitia muungozo huo wa Tume ya Utangazaji Zanzibar 2015, 

lakini baadhi yao huwa ndio chachu ya kuwagawa waandishi wa habari na wapiga kura wao kama njugu na kuwafanya kama leso mara baada ya kufikia kileleni. Wakati msaka tonge anapoitwa Muheshimiwa, kwako mwandishi wa habari ni adui mkubwa na hakumbuki tena ihsani uliyomfanyia, kwa muda wote wa kutafuta kula badala ya kura. 

Ifike muda mwandishi wa habari afahamu wajibu wake katika jamii, kuliko kukurupuka na mbio za sakafuni, ambapo mwishio huishia ukingoni. 

Kuacha kuupitia muongozo na kujuwa kilichoandikwa ndani ya muongozo huo ni khatari kwa chambo cha habari, na hasa katika kipindi ambapo vyomba vya habari humea kama uyoga kila uchao. kwa vile huu ni msimu kwa baadhi ya wanahabari, naomba niwatanabahishe kuwa “mwendatenzi na omo, hurejea ngamani”, kukimbia kwao kwenye chumba cha habari, 

kwa kuwa tu ati yupo na mkuu fualani, kimbilio lako la mwisho huenda ikawa ni majuto ya Mussa na Firauni. 

Ni aibu na fedha kwa waaandishi wa habari kuwa watumwa wa elimu na taaluma zao na ndio maana hata kwenye biblia imesema “musipowashinda waandishi na mafarisayo ufalme wa mungu hamutaupata” lakini pia kwenye biblia hiyo hiyo Yesu (Nabii Issa A.S) amesema “sikuja kutengua taurati bali kutimiza taurati, lakini tazama kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya taurati ya bwana kuwa ni uongo” Hayo ni maneno matakatifu kutoka kwenye biblia, lakini pia kwenye kur-an karimu Mwenyezimungu amesema hivi “ naapa kwa kalamu na yale wayandikayo (kwa kalamu hizo).

 Kwa kutumia vitabu hivyo vitakatifu, si dhani kama kuna mtu yoyote mwenye akili na ufahamu ambaye atapingana juu ya ukweli huo. Kwa kupitia baraha la hatari Tanzania, mwaka 2010 iliwahi kuchaopisha kitabu maalumu chenye Kanunu za maadili kwa wanahabri, ambapo imelezwa kuwa “mwandhishi wa habari anawajibu wa kueleza katika taarifa yake, mlolongo wa matukio yote kwa usahihi, uhakika na nuwazi kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari na sheria zilizopo, zinalinda haki na makundi maalumu”. 

Lakini pia, mwandishi wa habari anawajibika kupambanua lipi baya na zuri,katika utendaji wa kazi zake za kila siku, maoni au tarifa zake ni lazima zizingatia maadili, ukweli na usahihi wa habari yake kabla ya kuitoa au kuichapisha, hatuoshi tu kuangalia hayo , lakini apia apime athari na faida kwa jamii yake. 

Si hivyo tu, lakini pia, kuna baadhi ya waandishi wa habari nchini, wamekosa umaminifu katika kazi zao, na hasa ukiangalia kisingizo chao kikubwa kipato kitogo hakiendani na taaluma na kazi wanazofinya, na kama hilo lina ukweli kwa nini hutafuti kitu kingene chenye tija na ujira mzuri kuliko hii fani ya habari? Kama hilo ni jambo la kupelekea mwandishi wa habari kuingia kwenye majaribu, kwa nini asishawishi kuongezewa mshahara kama ambavyo amekuwa akipigia deba taasisi nyengine? 

Lakini ni jambo la ajabu sana kwa waandishi wa habari nchini ambao wengi wao hushia kwenye mikutano, semina, makongamano pamoja na mialiko ya kwenda kula na kunywa, kitu ambacho kinapeleka hata kusahau wajibu na haki zao za msingi kama waandishi wa habari na baadae kuwa leso kwa wala habari. 

Katika karne ya 19, magazeti na majarida mengi ya ulaya yalijikita kwenye kampeni juu ya masuala ya kijami na kisiasa, ikiwa ni mabadiliko ambayo kwao waliona ni katika kuwavutia wasoji wao. 

William Randolph Hearst na Joseph Pulitzer kwa uapande wao walijikita mara nyingi katika kuandika habari za kushtua jamii ambazo zaidi zilikuwa kwenye habari za uchunguzi, ambapo mara kadha walikuwa wakizungumzia juu ya uovu ulikuwa ukifanyika katika jamii zao. 

Ni kinyume na hapa kwetu anaweza akasifiwa mtu hata kama hana sifa ilimradi tu, awepo kwenye chombo cha habari. Kwa kuwa uandishi wa habari ni taalumu na fani maalumu kama zilivyo fani nyengine, kama vile sheria na udaktari, lakini ni jambo la kushangaza waliomo kwenye fani hii ya habari wengi wao hajuwi kitu kinachoitwa maadili, heshima wala utu wa mtu, kwao mshiko ndio kitu cha kwanza . 

Inasikitisha kuona Tanzania kuna taasisi nyingi za kihabari,lakini hakuna moja ambayo wanachama wake wamefikia malengo, labda majungu, fitna na uhasama ndio ambao huongoza taasisi hizo. 

Licha ya kwamba waandishi wa habari wapo mstari wambele kuwatetea wanasiasa, walimu, madaktari, lakini ni kichekisho kwamba wao wenyewe wameshindwa kujikomboa, licha ya kwamba kwa mataifa mengi uandishi ni muhimili wa nne katika mataifa hayo. Taasisi kama MCT, UTPC, MISA-TAN, TAMWA, PRESS CLUB, na jumuiya ngengine za kiahabari nchini zimekuwa mstari wa mbele katika kumtetea mwandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na kuchapisha vijitabu kuhusiana na masuala ya maadili ya waandishi wa habari pamoja na vyombo vyao lakini wapi. 

Bado mwandishi amebakia kuwa ni leso kwa wanaojuwa kuwatumia, ni lazima tufahamu kwamba kuna tofauti kubwa kati ya mwandishi na mwandishi wa habari, kwa kila mtu ni mandishi hata mwanasheri na daktari ni waandishi, lakini si waandishi wa habari, hii ni fani na yenye thamni kwa mwenye kujithamini.

Nasikitika kusema kwamba, waandishi wengi wa habari wa Tanzania hawajuwi umuhimu wao kama ambavyo msanii Mrisho Mpoto alivyo sema kwenye nyimbo yake ya “UHURU WANGU UKO WAPI” hii ni nyimbo maalumu kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini. Lau kama mwandishi wa habari angejuwa thamani yake kwa taifa na jamii kwa ujumla, asingekubali kuwa leso, nasema leso ni kwa sababu ni mara nagapi tumesikia kuna waandishi wameachwa kwenye misafara, kudhalishwa hata kupigwa.

 Jibu unaweza sema hapana, lakini ujiulize ni mara ngapi waandishi wameandika sakata la ESCROW, FEDHA KHARAMU, KASHIFA, WIZI NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMAH, cha ajabu waandishi wa habari wakatoa na jina ati “UFISADI”. Waandishi wa habari wanaogopa kusema Fulani mwizi , na ni kweli mwizi asikuchota vijisenti. Kwa kuwa kipindi ni cha mavuno, kitu cha kuzingatia ni kujiuliza unavuna nini?. Maadili katika kuandiaka au kuandaa habari za uchaguzi ni kitu cha msingi sana. 

Ni lazima tuzingatie kwamba, mtoa wa hutuma za utangazaji ni mtu aliyepewa leseni, anayetoa huduma ya utangazaji chini ya na kulingana na vifungu vya sheria na masharti ya leseni iliyotolewa na Tume. kwa mnasaba huu basi unaposoma sehemu ya kwanza ambayo imesishia kwenye uafafanuzi utaona sehemu kubwa imegusia Utangazaji ama Tv au Radio, hii ni kuonesha vyomba hivi ndio hutoa taarifa kwa haraka Zaidi kuliko vyengine. Kitu cha kuzingatia kwa sasa kila mtu awe na hadhari kuhusiana na kutangaza suala zima la uchaguzi nchini kwa ajili ya kudumisha Amani na utulivu nchini.

0 comments:

 
Top