LESO ni miongoni mwa kitu muhimu, katika maisha ya watu wa mwambao wa Afrika Mashariki, ijapokuwa mada yangu kuu sio Leso.

Neno LESO linaweza likawa na maana pana sana, kulingana na matumizi ya jamii husika, kwa mfano unapokutana na wenyeji wa Mombasa, Lamu au Pate nchini Kenya, neno  LESO lina maana ya Khanga lakini katika jamii ya Tanzania LESO si khanga na upo uwezekano wa kuna na matumizi tofauti na khanga.

Ifahamike kwamba lengo la makala hii sio kuwafananisha wa waandishi wa habari na LESO, lakini baadhi ya waandishi taasisi za kihabari nchini kutumika mithili ya leso na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchanguzi mkuu wa oktaba 2020.

Uzoefu unaonesha wazi kwamba kila ifikapo kipindi cha uchaguzi ama mandishi wa habari au chomba cha habari, huwa ni sehemu ya chama cha kiasiasa hivyo basi husahau wajibu wao na ndio maana Tume ya Utangazaji Zanzibar mwaka 2015, ilitoa kitabu maalumu cha Muongozo wa Huduma za Utangazaji Wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Muongozo huo wa 2015, umebainisha vipengele kadhaa ambavyo ni wajibu wa mwandishi wa habari au taasisi ya habari kama vile gazeti, Tv, radio au hata mitandao ya kijamii kuweza kuupitia, kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa mambo kwa mfano sehemu ya pili ya Muongozo huo umebainisha masuala ya midahalo ya kisiasa, matumizi ya simu katika vipindi, usawa katika utoaji wa habari na mengine kadha wa kadha.

Kwa kuwa muongozo huu wa Uchaguzi Mkuu umegawanywa katika sehemu tano ambapo katika Makala yetu hii tutaweza kugusia sehemu ya kwanza, ambapo imeeleza.

Muongozo huu utatumika na kuongoza watoaji wote wa huduma za utangazaji wanaofanya kazi Zanzibar, huku zikijumuisha uchaguzi mkuu, uchaguzi mdogo na uchaguzi wa marudio.

Katika kipengele hicho kwa hatua ya kwanza kimeeleza kitatumika kwa watoaji wa haduma za utangazaji waliopo Zanzibar. Iwe radio na Tv au  Online Tv ama  nyenginevyo kwa  kuwa vipo na kufanya shusghuli zake Zanzibar, muungozo huu unawahusu kwa njia moja ama nyengine.

Labada unaweza ukajiuliza kwa nini Utangazaji? Ni kwa sababu ni njia nyepesi kuweza kusambaza habari kwa haraka kulinganisha na gazeti au Tv.

Radio ni chombe pekee cha habari kinacho wafikia wananchi kwa haraka zaidi, kuliko chombo chengine chochote cha habari.

Wanasiasa wengine hutumia radio kuwasilisha  maudhui yao, yawe mazuri au mabaya. Wanasiasa walio wengine hutumia vyombo vya habari kama daraja la kumvusha upande wa pili, ila husahau kwamba wa ni sehemu ya jamii na ndio mtaji wao wa kupata kura, hivyo basi ni vyema kuangalia athari ya vyombo vya habari kabla ya hatari kutokea.

Mifano ipo mingi karibu kila pembe ya dunia, lakini funzo zuri lipo kwa nchini wanachama wa Mtengamano wa Afrika ya mashariki kama vile Kenya, Rwanda, Burudi, Sudan, na hata Ethiopia, vyombo vya habari ndio vilichangia katika kuchochea vurugu kwa ajili ya kuwaridhisha wanasiasa uchwara, waisiotakia mema nchi zao na ndio maana nikasema taaluamu ya habari ni tofauti na LESO.

Ingawaje muuongozo huu unatumika zaidi Zanzibar tu, hivyo ni vyema kuwafahamisha  mwandishi wa habari mipaka na wajibu wa kazi zao za kila siku.

Aidha waandishi wa habari na vyombo vya habari, ni jukumu lenu kuupitia muongozo uliotolewa na Tume ya Utangazaji Zanzibar (2015), kwa sababu unatumika katika nafasi zote za wagombea kama vile Urais, Uwawakilishi, Ugunge na Udiwani.

Kumfananaisha mwandishi wa habari na leso sio jambo jema, lakini katika kipindi hiki cha msimu wa uchaguzi wapo baadhi ya waandishi au vyombo vya habari nchini, hutumika kama leso. Na uchaguzi mkuu wa oktaba kwao ni msimu mzuri  wa mavuno kwa kupitia migongo ya wanasiasa ambao wana uchu wa madaraka .

Lakini pia ni wakati mwafaka kwa baadhi ya waandishi kutumia kalamu zao kwa kuwapotosha, kuwatia khofu au kuwatisha wasomaji, watazamaji wa tv au wasikilizaji wa radio, ili mradi watimize yale wanayotaka kwa muda mchache, na ndipo ninapowasisitiza kuupitia muongozo uliotolewa na Tume ya Utangazaji Zanzibar kwani kuna mambo mengi ya kujifunza pamoja na kuyafanyia kazi.

Aidha ndani ya muongozo huu kuna ufafanuzi wa mambo mbali mbali kama vile:~ Huduma ya habari  ndani ya muongozo umeeleza kwamba ni huduma inayotolewa wa sauti, data, maandishi au picha ama zikiwa za mnato au zinazojongea isipokuwa pale ambapo zinafanayika kwa mawasiliano binafasi.

Mbali na hilo ufafanuzi mwengine ni kuhusiana na Matangazo ya kisiasa ambapo muongozo umebainisha kwamba ni matangazo yaliyolipiwa na yanayokusudia kuendeleza maslahi ya chama chohote cha kisiasa.

0 comments:

 
Top