Mradi Mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya Abdulla Mzee iliyopo Mkoani Kisiwani Pemba tayari umeshaweka alama ya Kihistoria itakayoendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Jamuhuri ya Watu wa China na Zanzibar ambao una zaidi ya miaka 52 sasa.

Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania Bwana Lu Youqing alisema hayo wakati akipokea salamu za shukrani kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizowasilishwa kwake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mtaa wa Namanga Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam.

Balozi Lu alisema Serikali ya nchi yake kwa makusudi imeamua kufanya ushirikiano wa kina na wa ndani kati yake na Zanzibar kutokana na Viongozi Wakuu wa pande hizo mbili kuasisi mafungano hayo yenye kuleta faraja na upendo baina ya wananchi wa sehemu hizo mbili.

Alisema upo ushahidi wa wazi unaothibitisha ushirikiano wa pande hizo mbili ukijikita zaidi katika uanzishwaji wa miradi ya maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii Visiwani Zanzibar na kuungwa mkono wa kiuwezeshaji na ndugu zao hao nwa Jamuhuri ya Watu wa China.

Balozi Lu Youqing alielezea faraja yake kutokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia ya Kisasa yanayoendelea kupamba moto ndani ya Visiwa vya Zanzibar jambo ambalo hukleta matumaini kwa Wananchi wake hawa Vijana.

Akizungumzia utanuzi wa eneo la maegesho ya ndege katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar {Terminal 2 } Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing alisema hakuna matatizo yoyote katika uendelezaji wa mradi huo kwa Vile Benki ya Kimataifa ya Exim imeshapata njia ya kupata fedha kwa ajili ya kukamilisha wa mradi huo.

Balozi Lu Youqin kilichochelewesha kuendelea kukamilika kwa mradi huo ni mabadiliko yaliyotokea ya Uongozi wa Benki ya Exim yaliyokwenda sambamba na mabadiliko mengine ya Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipamgo ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndio mratibu wa mradi huo wa Kimataifa.

Bwana Lu Youqing alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China utatoa kipaumbele ombi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la ujenzi wa Nyumba za Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee Mkoani.

Alisema kipaumbele hicho kitaingizwa katika mipango inayokusudiwa kutekelezwa na China katika kipindi cha mwaka ujao kupitia mpango wake wa kuunga mkono mataifa ya Bara la Afrika.

Mapema akitoa ashukrani kwa niaba ya Serikali ya Ma9induzi ya Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alieleza kwamba kazi inayofuatia kwa sasa na kutafuta mbinu za ujenzi wa nyumba za Madaktari katika Hos9itali ya Abdulla Mzee.

Balozi Seif Alisema kazi hiyo itakwenda sambamba na Serikali kujitahidi kutafuta madaktari mabingwa watakaoweza kutoa huduma za afya kulingana na mahitaji halisi ya wagonjwa ndani ya Kisiwa cha Pemba pamoja na maeneo jirani yaliyokuzunguuka kisiwa hicho.

Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar ameelezea faraja yake kutoka na hatua kubwa na ya mwisho ilizofikiwa na wahandisi wa ujenzi wa Hospitali hiyo itakayokuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi walio wengi.

Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani imejengwa katika mfumo wa teknolojia ya kisasa utakaokuwa na uwezo wa kutoa huduma mbali mbali ikiwemo zile za upasuaji mkubwa, uchunguzi wa maradhi mbali mbali itaweza kukidhi mahitaji ya huduma za Kiafya kwa wancchi walio wengi ndani ya Visiwa vya Zanzibar pamoja na ukanda wa mwambao wa Tanzania.

Wagonjwa wapatao 130 wanaweza kulazwa kwa wakati mmoja kwenye Hospitali hiyo zikiwemo huduma zote muhimu kama vyumba Vitatu vya upasuaji, chumba cha wagonjwa mahututi { ICU }, Wodi ya wazazi pamoja na jengo la msikiti litakalotumiwa na wagonjwa pamoja na familia zao kwa ajili ya ibada.

Balozi Seif alitumia mazungumzo hayo kuishukuru pia Serikali ya
Jamuhuri ya Watu wa China kwa kukubali kugharamia ujenzi wa uwanja wa michezo wa Mao Tse Tung uliopo Mperani Kikwajuni Mjini Zanzibar. Alisema ujenzi wa uwanja huo utasaidia kurejesha hadhi ya jina la Kiongozi na muasisi wa Taifa hilo lilioko katika Bara la Asia.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top