Na Jumbe Ismailly-Itigi
SERIKALI inaangalia uwezekano wa kuongeza adhabu ya faini mara mbili zaidi ya inayotozwa kwa wamiliki wa magari makubwa ya mizigo wanaokwepa kuingia kwenye mizani kwa ajili ya kupima mizigo waliyobeba.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni wakati akitembelea kukagua ujenzi wa mizani ya kupima uzito wa magari inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi aug,mwaka huu.

Aidha Naibu waziri huyo alisema lengo la hatua hiyo ni kuwafilisi kabisa wenye magari hayo wanaozidisha uzito wa mizigo na kuchangia serikali kupata hasara kubwa kutokana na uharibifu wa barabara.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo wakati umefika sasa wa kuangalia upya adhabu ya faini inayotozwa kwa magari yanayokwepa kupima uzito wa mizigo iliyobeba kutokana na idadi kubwa ya madereva kuonekana kutoijali na kuidharua kwa kuwa ni ndogo ukilinganisha na uharibifu wa barabara wanaoufanya.

Katika hatua nyingine akiongea na watendaji wa TANROADS Mkoa wa Singida pamoja na Wakandarasi wanaotengeneza barabara ya Manyoni-Itigi –Chaya kwenye ukumbi wa Hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Gasper mjini Itigi,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani amesema ili kukabiliana na wizi wa miundombinu ya barabara,Halmashauri ya Itigi haina budi kushirikiana na watendaji wa wizara hiyo kuwabaini wahalifu kwani serikali imetumia fedha nyingi kujenga barabara hiyo,vile vile amewaeleza Wakandarasi sababu za kuchelewa kuwalipa malipo yao inatokana na serikali kukabiliwa na majukumu makubwa,lakini hakusita kuwaahidi kuwapatia malipo yao.

Katika taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Manyoni –Itigi- Chaya yenye urefu wa kilomita 89.30 inayojengwa kwa kiwango cha lami iliyotolewa kwa Naibu waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida,Leornad Kapongo inasema kuwa ujenzi wa barabara hiyo inayogharamiwa na serikali kwa asilimia mia moja utagharimu shilingi 109,642,609,872/=.

“Mkataba wa usanifu na ujenzi wa barabara hii unagharamiwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja”alifafanua Mhandisi Kapongo.

Hata hivyo Meneja huyo wa Mkoa aliweka bayana akuwa mradi huo ulitiwa saini kati ya TANROADS kwa niaba ya serikali na Mkandarasi M/s SINOHYDRO Corporation Ltd.kutoka China julai,30,2010 kwa gharama ya shilingi 109,642,609,872/= kwa utekelezaji wa miezi 36 pamoja na kipindi cha uangalizi cha miaka mitatu baada ya ujenzi.

“Kwa upande wa mkataba wa usimamizi wa ujenzi wa barabara hii,ulitiwa saini kati ya TANROADS na Kampuni ya kihandisi ya kigeni ya Nicholas O’Dwyer @Compan Ltd kutoka nchini Ireland kwa kushirikiana na kampuni ya kihandisi ya kizalendo ya Apex Engineering Co,Ltd ya Dar-es-Salaam Apr,14,2011 kwa gharama ya shilingi 3,913,970,000/=” alifafanua

0 comments:

 
Top