Na Jumbe Ismailly-Ikungi
MKUU wa wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida amewaagiza maafisa watendaji wa kata na vijiji wilayani hapa kusimamia kwa karibu sana uanzishwaji wa mabaraza ya wazee na kuhakikisha mabaraza hayo yanaanzishwa kwenye maeneo yao na hatimaye waweze kuunda baraza la wazee la wilaya hiyo.

Akizungumza na wazee maarufu wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya Ikungi,Mkuu huyo wa wilaya,Miraji Mtaturu alisema kuwepo kwa mabaraza hayo katika ngazi za chini yatasaidia kuzishauri shughuli za serikali.

Alibainisha Mtaturu kwamba asilimia kubwa ya wazee hao ni wastaafu na watu wenye taaluma zao na kutoa mfano uwepo wa wataalamu wa kilimo utasaidia kuwawezesha wakulima waliopo kwenye maeneo yao kulima kwa kufuata ushauri wa wataalamu hao.

Kufuatia ushauri huo wa kuanzisha kwa mabaraza ya wazee katika ngazi zote,wazee hao alisema baada ya utawala wa mwalimu Julius Nyerere wazee walisahaulika,jambo ambalo limeanza kurudisha heshima katika pande zote mbili.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida ameanzisha utaratibu wa kukutana na wazee maarufu wa wilaya hiyo kwa lengo la kufahamiana na kupeana mikakati ya kujiletea maendeleo yao.

0 comments:

 
Top