Na,Jumbe Ismailly-Singida
KANISA la Assemblies of God Tanzania (TAG) limewapatia waangalizi wa majimbo 33 nchini ya Kanisa hilo,ili kuwawezesha kufanikisha utekelezaji wa malengo makuu kumi ya dira ya maendeleo ya kanisa hilo,ili ifikapo mwaka 2018, utekelezaji wa malengo hayo yote yawe yamekamilika.

Msaada huo wa usafiri wa pikipiki 400 kwa nchi nzima umegharimu kati ya shilingi milioni 12 na milioni 16 kutokana na pikipiki moja kununuliwa kwa bei ya wastani wa kati ya shilingi milioni tatu na milioni nne.

Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG,John Mtokambali aliyasema hayo kwenye halfa ya kukabidhi pikipiki 400 kwa waangalizi wa makanisa ya TAG Tanzania,hafla ambayo ilifanyika katika kanisa la TAG Mandewa,mjini Singida.

“Na tumetoa pikipiki hizi kwa makusudi makubwa matatu,kwanza kila mwangalizi ambaye ni kama mkuu wa wilaya wa kanisa letu anao wajibu wa kikanisa anao wajibu wa kikatiba,kutambua kwamba pikipiki hizi zitaharakisha kuwapa wepesi wa kuharakisha utekelezaji wa majukumu yao”alifafanua.

Kwa mujibu wa Askofu huyo jukumu la pili ni kuwezesha utekelezaji wa diya ya maendeleo ya kanisa letu,kanisa letu lina dira ya maendeleo yenye malengo makuu kumi ambayo yanalenga ifikapo mwaka 2018 malengo hayo yote yawe yamekamilika.

Mapema akizuzngumza na waumini wa madhehebu ya Kanisa hilo la TAG Mkoani Singida,Katibu Tawala Msaidizi kitengo cha maji,Mhandisi,Lidya Joseph aliwahimiza zaidi waumini wa madhehebu ya dini mbali mbali juu ya umuhimu wa kuhubiri amani,utii pamoja na kuwajibika kwa wananchi wao.

“Kwa kweli sisi kama serikali tunasisitiza sana watu wa madhehebu ya dini waendelee kuhubiri amani,wahubiri utii pamoja na kuwajibika kwa wananchi na tunawapongeza sana kwa hatua hii ambapo nimeelezwa kuwa pikipiki hizi ni kwa ajili ya watendakazi wa kanisa,basi waendelee kuwa na juhudi katika kuwahimiza washirika wao ili wawe raia wema na waendelee kulitumikia vizuri jamuhuri ya muungano wa Tanzania”alisisitiza mwakilishi huyo wa serikali.

Akizungumza kwa niaba ya waangalizi waliopokea usafiri huo wa pikipiki,Mchungaji Kalebi Patrick Maumbuka wa kanisa la TAG,Ikungi Mkoani Singida alisema usafiri huo wa pikipiki utawasaidia sana kutangaza neno la Mungu kwa haraka zaidi,kwani awali walikuwa wakitegemea usafiri wa mabasi ambayo yalichangia kuwakwamisha kufikisha ujumbe wa neno la mungu kwa wakati muafaka.

0 comments:

 
Top