Na Jumbe Ismailly-Manyoni

TAASISI ya Kikristo kutoka nchini Ujerumani (DIFAEM) inayojishughulisha na huduma zaa dawa,imeipatia Hospitali ya Misheni Kilimatinde,wilayani Manyoni,Mkoani Singida maabara ndogo ya kupimia ubora wa dawa ili kubaini dawa bandia zitakazokuwa zikiuzwa katika vituo vya kutolea huduma za afya katika wilaya hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mfamasia wa Misheni,DRV,Elisabeth Schenk katika Kijiji cha Ntope,tarafa ya Nkonko,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati wa ugawaji wa mahindi ya msaada kwa watu wanaohofiwa kupoteza maisha yao kwa kutokuwa na chakula cha kuwasaidia wakati wa kilimo cha msimu wa masika ya mwaka huu.

“Nimeomba kuipata huduma hii kwa sababu ninapenda kuhakikisha kwamba dawa tunazozitoa katika vituo vyetu vya kutolea huduma ni dawa zenye ubora na wala siyo dawa za bandia”alisisitiza Mfamasia Schenk.

Aidha Mfamasia huyo alifafanua kwamba taasisi hiyo iliipatia Hospitali hiyo ya misheni Kilimatinde maabara hiyo tangu mwezi Nov,mwaka jana,na kwamba Hospitali hiyo ni hospitali pekee Mkoani Singida yenye huduma ya aina hiyo.

Hata hivyo Schenk aliweka wazi kwamba tangu maabara hiyo ilipoanza kutoa huduma zake katika Hospitali hiyo imesaidia kuhakikisha kuwa dawa nyingi zinazotolewa kuwa ni dawa nzuri na kuwaondolea mashaka kwa dawa ambazo walikuwa wakifikiria kuwa nibandia.

“Kwa mtu yeyote yule ambaye ana mashaka na dawa zake,hususani katika vituo vya afya,zahanati,Hospitali pamoja na duka la dawa muhimu au pharmacy wanaweza kutuletea sampuli ya dawa na tunaweza kupima”alifafanua mfamasia huyo.

Akibainisha zaidi Mfamasia huyo alisema tangu shughuli za maabara ndogo ya kupima dawa zilipoanza endapo watagundua dawa zisizokuwa na ubora,hatua hufuatwa wakati stock ya dawa hiyo ikiwa imewekwa kando,maabara kubwa yenye nafasi zaidi za kupima(vipimo maalumu)itapima dawa hiyo na shirika la viwango Tanzania (TFDA) inaendelea kuchukua hatua na kuwasiliana na Kampuni na Distributors.

Nyingine ni mtu mwingine apime dawa hiyo tena,maabara aina hiyo (minlab)ipime dawa hiyo na mamlaka kama vile TFDA zijulishwe pamoja na watendaji wote katika Minlab hiyo wajulishwe kwa njia ya mtandao.

“Kwa sababu kuna reagents za kununua,vituo vingine vinatakiwa kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya vipimo”alibainisha mfamasia huyo.

0 comments:

 
Top