Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi amesema kwamba upo ulazima kwa akinamama Nchini kuchangamkia maisha na kuacha tabia ya kusubiri akina Baba katika maamuzi ya familia kutokana na mabadilido ya Dunia yaliyopo hivi sasa.

Alisema Akinamama wanapaswa kuelewa kwamba wao ndio nguvu ya f amilia inayopaswa kutafutiwa nyenzo na Mikakati mbali mbali ya kuendesha maisha yao kila siku.

Mama Asha Suleiman Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Akina Mama pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Vikunguni mara baada ya kukagua Kituo cha Afya cha Kijiji nhicho kilimo ndani ya Sherhia ya Ng’ambwa Jimbo la Ole Wilaya ya Chake chake Kisiwani Pemba.

Alisema uamuzi wao wa kuunda Vikundi vya ushirika umekuja wakati muwafaka kwa vile hakuna njia ya mkato ya kusaidia kujiongezea Kipato cha kuwahudumia watoto wao hasa katika masuala ya Kielimu.

Mama Asha aliwanasihi akina Mama pamoja na Wananachi wa Majimbo la Kisiwa cha Pemba kuacha mazoea ya kuwapa madaraka Watu wasio nania sahihi ya kuwasimamia katika maendeleo yao.

Alisema Viongozi wa Majimbo katika nafasi ya Ubunge na Uwakilishi wametengewa mifuko ya Jimbo iliyolenga kuwapa nguvu za kuwawezesha kuendesha miradi ya Wananchi katika Maeneo yao lakini wengi kati yao wanashindwa kusimamia kazi hiyo na badala yake kuhama kwenyen Majimbo yao mara baada ya kuchaguliwa na Wananachi.

Mama Asha aliahidi kuvisaidia vikundi vya Ushirika vya Kijiji cha
Vikunguni mara baada ya kukamilika kwa harakati za Uchaguzi Mkuu na kuwasisitiza umuhimu wa kuendeleza Amani iliyopo Nchini.

Amesema Wananchi na hasa akina Mama Nchini wanapaswa kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais wa Sasa Dr. Ali Mohammed Shein kwa uamuzi wake wa kusimamia kwa nguvu zote amani inayoendelea kushamiri hivi sasa.

Mama Asha alifahamisha kwamba cheche ya vurugu zinazoonekana kuashiriwa hasa na Vijana katika baadhi ya maeneo nchini zinatokana na baadhi ya Vijana wanaohusika na ishara hiyo kukosa ucha mungu.

Alieleza kwamba Imani ya Dini miongoni mwa Wananchi hasa kundi hilo la Vijana imepungua na kusababisha baadhi ya vijana kuwa na dalili ya maamuzi ya kutaka kufanya fujo hatma yake inaweza kuitumbukiza Nchi katika vurugu zisizo na ulazima wowote.

Mapema Kiongozi wa Vikundi vya Ushirika vua Kijiji cha Vikunguni Bibi Fatma Mohammed Ali alisema hadi sasa Kijiji hicho kimefanikiwa kuwa na Vikundi vya Ushirika Vinne lakini kilichopata usajili ni Kikundi cha Jipe Moyo.

Bibi Fatma aliziomba taasisi zinazohusika kusaidia elimu ya Ushirika itakayosaidia kuviwezesha vikundi vilivyobakia vya Maslahi kwa Wote, Tujiendeleze Mwanzo Mgumu kupata usajili wa kudumu na kuendesha shughuli zao katika taratibu za kisheria zinazokubalika.

Alisema ili kuvijengea mazingira ya uzalishaji vikundi hivyo umefika wakati kwa Viongozi pamoja na Taasisi za fedha kutoa mikopo kwavikundi hivyo mara baada ya kupata Taaluma inayokusudiwa ya kuendeshavikundi hivyo.

Akitoa salamu katika hafla hiyo fupi Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Bibi Hanuna Ibrahim Masoud alisema Kituo cha Afya cha Kijiji cha Vikunguni kilichoanzishwa kwa Nguvu za Wananachi wenyewe kilipata msukumo mkubwa katika ujenzi wake uliotolewa na aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo Mh. Hamad Rashid Mohammed.

Hata hivyo Bibi hanuna alisema jitihada hizo zilipata changamoto kubwa ya mvutano wa umiliki wa Kituo hicho kutoka kwa makundi mbali mbali uliosababisha uzoroteshaji wa ukamilishaji wa ujenzi wake.

Alisema mvutano huo ulichukuwa muda mrefu hali iliyopelekea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufika kusikiliza mzozo huo na kuwaahidi Wananachi wa Vikunguni kuwatafutia wafadhili wa kukamilisha ujenzi wa Kituo hicho.

Bibi Hanuna Ibrahim Masoud alifahamisha kwamba juhudi za Balozi Seif zilipelekea kupatikana kwa Kampuni ya Milele iliyokubali kusaidia kukamilisha Ujenzi huo.

Alieleza kuwa Kampuni hiyo kwa nia ya kuunga mkono jitihada za
Wananchi hao za kupata huduma za Afya ikajitolea pia kujenga Nyumba ya Daktari sambamba na kufanya marekebisho makubwa zaidi ya ujenzi wa jengo la Kituo hicho litakalokuwa na uwezo kamili wa kutoa huduma nyingi zikiwemo zile la Akina Mama wajawazito na Watoto.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Chake chake kwa niaba ya Wananachi wa Wilaya hiyo hasa wale wa Kijiji husika cha Vikunguni alimpongeza Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar kwa kukamilisha ahadi aliyotoa kwa Wananchi hao wakati alipotenmbelea mwaka uliopita.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top