Na,Jumbe Ismailly-Iramba

BAADA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupuliza kipyenga cha kuwaruhusu wanachama wake kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge na udiwani,Naibu Waziri wa Fedha,Lameck Nchemba Mwigulu ameanza kutoa vitisho kwa wagombea wengine wa nafasi hiyo.

Mwigulu ameanza kutoa vitisho hivyo baada ya kupata habari kutoka kwa wapembe wake kwamba kuna mgombea mmoja wa chama hicho aliyechukua fomu ya kugombea ubunge ametangaza kuwanunua wapambe wake ili aweze kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa mujibu wa Mwigulu mgombea yeyote yule aliyeandaa pesa nyingi kwa ajili ya kuwaanunua mawakala wake,vile vile anatakiwa kuandaa majibu juu ya pesa hizo nyingi amezipata wapi.

“Wengine wanasema wameandaa pesa nyingi kununua mawakala wangu,mimi niwaambie aliyeandaa pesa nyingi kunua mawakala wangu anatakiwa pia aandae majibu juu ya hizo pesa nyingi amezitoa wapi?”alihoji Mwigulu huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Huku akijifananisha na hayati Moringe Sokoine,Mwigulu ambaye amewahi kushika nafasi ya Naibu katibu mkuu wa CCM Taifa,hakusita kuwatahadharisha baadhi ya wagombea wa nafasi hiyo kwamba wasidhani watu wale waliokuwa wakimwita Sokoine wa pili wanamtania,badala yake wajiandae kutoa maelezo ya kule walikozipatia pesa hizo za kuwanunua mawakala wake ili aweze kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho.

“Anadhania wale waliokuwa wananiita Sokoine wa pili walikuwa wanatania,hivyo anayesema ameandaa pesa nyingi atanunua mawakala wangu aandae pia majibu kwamba hizo pesa nyingi amezitoa wapi”alisisitiza huku akiwaangalia wananchi kwa hasira.

Aidha Mwigulu aliyeonyesha kukerwa na kauli ya mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo,hata hivyo hakusita kutoa vitisho kwa wapinzani wake kwamba unapotangaza vita huku ukiwa kwenye nyumba ya vioo unatakiwa pia ujitathimini sana.

Huku akijiamini kuibuka na ushindi,mgombea huyo alisisitiza pia kwamba kutokana na kazi zilizofanyika wakati wa kipindi cha uongozi wake,hivyo ana uhakika wa kuibuka kidedea katika mpambano huo.

“Na taasisi zetu zinazosimamia uchaguzi zitasimamia,na taasisi zetu zinazosimamia maadili zitasimamia,lakini baada ya uchaguzi aliyeandaa pesa nyingi za kununua mawakala wangu aandae pia na majibu kwamba pesa zile amezitoa wapi”.alisisitiza Mwigulu.

Hata hivyo Naibu waziri huyo wa fedha aliweka bayana kwamba kuandaa pesa siyo tatizo bali kuandaa majibu ya mtazania maskini anayetokea eneo maskini ambako watu wanaokula mlo mmoja wamechanagia maabara hiyo pesa nyingi ikiwa haipo,lakini ya kununua mawakala wote itatoka wapi,ili watanzania waweze kufahamu inakotoka pesa hiyo isiyoweza kuchangia maendeleo na badala yake kununua mawakala.

Akimkabidhi fomu baada ya kulipa shilingi milioni nne,zikiwemo shilingi laki moja za fomu na 3,900,000/= za kuchangia chama,katibu wa CCM wilaya ya Iramba na mkurugenzi wa uchaguzi wilaya ya Iramba,Mathiasi Shidagisha alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha wapembe wa wagombea wote kuacha lucha za kukashifiana.

“Kuanzia tarehe 20 tutaanza kazi ya kuwatembeza hawa wakubwa na nimewaambia waliokuja kuwa hatutaki kashfa wala kukashifu mwenzake…na Mh Mwigulu najua ni Mbunge wetu lakini ubunge wako sasa hivi unaanza upya tena ninaruhusu ufanyekazi kuanzia leo na tutawazungusha matawi yote 135”alifafanua Shidagisha.

0 comments:

 
Top