WANAUME NA NGUVU ZA KIUME
Wanaume wengi walioacha kuvuta sigara wameacha siyo kwa kuogopa magonjwa ya moyo na saratani,bali kilichowashituwa ni kuelezwa kuwa sigara hupunguza nguvu za kiume-hapo ndipo palipoleta usikivu wa kuacha sigara.

“Smoking reduces blood and causea impotence”onyo kama hilo likiwekwa kwenye paketi za sigara Tanzania litapunguza idadi ya wavutaji.

Kwa kuyatambua madhara hayo pamoja na mengine mengi,ndipo Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone amekuwa akisisitiza wataalamu wa kilimo kutohamasiaha zao la tumbaku kulimwa katika Mkoa huo,kati ya mazao ya biashara yaliyopewa kipaumbele.

Pamoja na madhara hayo kuwepo kwa watumiaji wa tumbaku,lakini bado wakulima wa wilaya ya Manyoni wanaendeleza kilimo cha zao hilo mwaka hadi mwaka.

Wakulima wa zao la tumbaku wa Chama Kikuu cha Wakulima kanda ya kati (CETCU) Mkoa wa tumbaku Manyoni walifanya sherehe za ufunguzi wa masoko ya ununuzi tumbaku kwa mwaka 2014/2015 kwenye Chama cha msingi cha ushirika Msemembo,wilayani Manyoni,Mkoani Singida,na kuhudhuriwa na idadi ndogo ya wakulima wa zao hilo,licha ya kuwepo vikundi vya ngoma vya kabila la wasukuma,vilivyowaburudisha wananchi,wakulima,wanachama wa vyama vya ushirika pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

Katika sherehe hizo mambo mbalimbali yalizungumziwa ikiwemo changamoto zilizo nje ya uwezo wa chama,ambazo ni pamoja na kampeni ya kimataifa ya kupinga uvutaji wa sigara,hali ya hewa ya ukame inayolikabili eneo la kilimo cha zao la tumbaku mara kwa mara na kutokuwepo kwa sheria ya kumbana mchoma mkaa kushiriki katika zoezi la upandaji miti.

Changamoto zilizo ndani ya uwezo wa chama ni pamoja na tabia ya kutorosha tumbaku bado inaendelea miongoni mwa baadhi ya wanachama.Utoroshaji huo unachangia kwa kiwango fulani uzoroteshaji wa urejeshaji deni la baadhi ya wakulima wasio waaminifu.

Katika Makala hii Mwenyekiti wa CETCU LTD,Bwana Florence Mpanda katika risala ya wakulima wa tumbakau wa Chama kikuu cha wakulima Kanda ya kati kwa mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Bi Fatuma Hassani Toufiq kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku zilizofanyika katika Chama cha Msingi cha Ushirika Msemembo anazungumzia hali ya uzalishaji wa tumbaku,taarifa ya uzalishaji kuanzia msimu wa 2010/2011 hadi 2013/2014 pamoja na mchango wa maendeleo ya kilimo cha tumbaku kwa wakulima wa tumbakau katika eneo hilo.



0 comments:

 
Top