Na,Jumbe Ismailly,Ikungi
SHULE ya sekondari ya kata ya Ikungi,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida ipo hatarini kufungwa wakati wowote kutokana na kukosa choo cha wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo kwa muda mrefu sasa.
Katibu wa CCM wilaya ya Ikungi,Aluu Ismaili Segamba alitoa kauli hiyo kwenye mkutaano wa hadhara uliofanyikaa kwenye viwanja vya ghala vilivyopo katika mji mdogo wa Ikungi.
Aidha Segamba alifafanua kuwa hali ya shule ya sekondari Ikungi hivi sasa ni mbaya sana kutokana na wanafunzi pamoja na walimu wao kutokuwa na sehemu za kujisaidia kufuatia viongozi na wazazi wa shule hiyo kushindwa kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.
“Akazungumza Sigamba na magamba sijui na kitu gani tumeenda shule,kwanza nikiri ni kweli nimeenda kwenye shule ya sekondari ya Ikungi nimekula chakula na wanafunzi na walimu,lakini hali ya shule ya sekondari ya Ikungi ni mbaya shule itafungwa kwa kukosa vyoo”alisema kwa kujiamini Segemba.
“Kama wazazi mpo hapa,kweli siyo kweli…kweliii,shule itafungwa pale kwa kukosa vyoo halafu mna mbunge anakataza michango,sasa pale naenda kujisaidia mimi au watoto wenu?”alihoji katibu huyo huku akionyesha kukerwa na hali hiyo.
Alisema shule kukosa vyoo ni suala la aibu wanafunzi pale wa kidato cha nne na tano hawana pakujisaidia,halafu anakuja kulalamika kuwa katibu wa CCM ameenda pale shuleni kutafuta kura,jambo ambalo hakuwa tayari kukubalinanaalo.
Naye Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ikungi (MNEC),Jonathani Njau aliwakumbusha wakazi wa kata ya Ikungi juu ya umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura,ili wakati ukifika wajitokeza pia kupiga kura.
“Lakini tunatakiwa tukajiandikishe kwa wale ambao tuna sifa
ya kupiga kura,kwani watu wengi wanadhani zoezi la kujiandikisha ni la kisiasa siasa tu,la mzahamzaha si kweli.”alisisitiza mjumbe huyo.
Hata hivyo Njau pamoja na kutokuwepo kwa mikakati yeyote madhubuti ya kulirudisha jimbo hilo kutoka CHADEMA,lakini alijikuta akitamba kuwa mwaka huu CCM bado kitashinda na hapo Ikungi ndiyo watashinda zaidi.
“Kama mlidanganywa zile sarakasi za 2010 mwaka huu hakuna,hazitakuwepo na rafiki zangu,nawabip vijana wa Ikungi kuwa uhuni mlioufanya mwaka 2010,mwaka huu mlie tu,CCM ya mwaka huu imejitosheleza”alisisitiza Njau.
0 comments:
Post a Comment