Shirika la Hoteli la Wyndham, ambalo linaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya hoteli na moja kati ya vitengo vitatu vya kibiashara vya Kampuni ya Wyndham Worldwide, leo limetangaza kufunguliwa kwa Ramada Resort yenye vyumba 139 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Ufunguzi huu unaongezea kwenye hoteli nyingine nchini Morocco, Ghana, Nigeria na Tunisia, na kuendeleza upanuzi wa hoteli ya Wyndham katika kanda ya Afrika Mashariki. Pia hii ni hoteli ya kwanza AfriKa kuendeshwa kupitia kitengo cha usimamizi cha kampuni kinachoendelea kukua.

“Ufunguzi wa Ramada Resort jijini Dar es Salaam una umuhimu mkubwa kimkakati kwetu” alisema Bw. Dan Ruff, ambaye ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli ya Wyndham katika eneo la Ulaya, Mashariki ya Kati, AfriKa na Bahari ya Hindi. Aliendelea kusema, “Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya malazi yenye ubora wa kimataifa katika Afrika Mashariki, pamoja na dhamira yetu ya kuwa karibu na wageni na wateja wetu kupitia upanuzi katika kitengo cha usimamizi wa mali, hii ni hatua muhimu sana katika ukuaji wetu katika kanda hii. "

Pia Ruff alisema, “Ramada Resort ya Jijini Dar es Salaam, yenye vifaa vya kipekee na iliyoo kwenye eneo lenye mandhari mazuri ya ufukweni, imeweka viwango vipya kwa mahoteli yenye kiwango cha kati nchini Tanzania na tuna hamu ya kuwakaribisha wageni wetu wa kwanza kwa ukarimu wa kipekee wa Ramada”

Kati ya jumla ya vyumba 139, vyumba 117 ni vyenye ubora mkubwa na viko mkabala na ufukwe au na bustani, vyumba 21 ni vya kiwango cha hadhi ya juu na chumba kimoja cha hadhi ya ‘presidential suite’. Vyumba vyote vina TV aina ya flatscreen na channel za satellite na mtandao wa Wi-Fi unapatikana bila malipo. Kadhalika, kuna baa ndogo, vifaa vya kukuwezesha kujitengenezea chai au kahawa na bafu binafsi vyumbani. Sanaa za michoro ya Tinga-tinga inaongezea mandhari ya Afrika mashariki.

Vifaa vya burudani ni pamoja na bwawa la kuogelea, gym yenye vifaa vya kisasa na njia ya moja kwa moja inayoelekea ufukweni wa mchanga tifutifu. Kwa wateja wenye mikutano au matukio, tuna vyumba saba vya mikutano vinavyoweza kukaliwa na hadi watu 375 na maeneo matano ya vyakula na vinywaji yanayoandaa vyakula aina mbalimbali vya kiafrika na kimataifa vile vile.



Tangu ujenzi ulipoanza 2009, tumezingatia mipango endelevu ikiwemo kutibu na kutumia upya asilimia 100 ya maji taka. Tumesistiza kutumia maji yaliyotumika kwa asilimia 100, matumizi ya nishati ya jua, kutumia mwanga wa taa za LED na ulinzi wa ufukwe ili usimommonyoke. Pia Hoteli inapanga jinsi ya kutumia mabaki ya chakula kama virutubisho kwa ajili ya kukuza mbogakwa ajili ya matumizi ya Hoteli, bustani hiyo iko katika Ghorofa ya juu kabisa ya Hoteli. 


Bw. Murtaza Fazal, mmiliki wa Ramada Dar Es Salaam, alisema “Ninafurahi kusaini mkataba wa muda mrefu na Wyndham Hotel Group, kampuni yenye Hoteli Kubwa duniani. Pia najivunia kuwa mwekezaji wa kwanza kuitambulisha Ramada katika soko la Afrika Mashariki. Ninaamini kuwa hii Ramada mpya iliyoko katika ufukwe wa Jangwani itakuwa ni kimbilio la wenyeji na hata watalii wa kimataifa na wageni wa kibiashara, tunajivunia mazingira bora, ubunifu na huduma bora. 
“Najivunia pia kuwa mwanzilishi wa matumizi ya nishati mbadala ili kulinda mazingira, ni matumaini yangu kuwa wamiliki wengine wa Hoteli watakuwa waiga mfano” Aliongeza Fazal,.

Wageni watakaokaa katika hoteli ya Ramada Resort Dar es Salaam ambao ni wanachama wa Wyndham Rewards®, mpango wa kujiunga bure wa kuzawadia uaminifu wa wageni wa Ramada, wataweza kupata alama za thamani wakati wa ukaaji wao. Zawadi hizo ni kama vile malazi na chakula bila malipo, tiketi ya ndege bila malipo

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf Wyndham Hotel Group.

0 comments:

 
Top