Tunathamini mchango wako katika kusambaza taarifa za tamasha ulimwengu mzima. Sauti za Busara, tamasha la muziki maarufu Afrika Mashariki na lenye sifa kimataifa, litawaleta wasanii mbalimbali katika toleo la tamasha la 12 mwakani, tarehe 12 – 15 Februari mjini Zanzibar.

katika kusherekea utofauti na uzuri wa muziki wa kiafrika, Sauti za Busara huvutia wageni kutoka sehemu zote za Afrika na kwingineko kusikiliza muziki wa African roots, fusion, pop, soul, Taarab, rap, reggae na aina nyingine nyingi, yote ikipigwa live kwa asilimia 100. Sauti za Busara 2015 itawaleta; Alikiba, Msafiri Zawose, Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band kutoka Tanzania, Blitz the Ambassador kutoka Ghana/USA, Octopizzo and band na Sarabi kutoka Kenya, Ihhashi Elimhlophe na The Brother Moves On kutoka South Africa, Tcheka kutoka Cape Verde, Diabel Cissokho kutoka Senegal, Loryzine kutoka RĂ©union/France naMgodro Group kutoka Zanzibar and more.

As a dynamic platform that brings global citizens together, Sauti za Busara values and appreciate TanzLikiwa kama jukwaa lenye kubadilika na kuwakutanisha wenyeji na wageni pamoja, Sauti za Busara inathamini na kutambua Tanzania kama nchi yenye amani duniani. Huku 2015 ikiwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu Tanzania, tunaamini kwamba ili maendeleo ya taifa yaendelee bila vizuizi, tunahitaji kuimarisha umoja, kuheshimu utofauti wa watu/vitu mbalimbali na kufanya kazi ili kutunza na kulinda amani hii yenye thamani. Tamasha pamoja na wadhamini wamezindua shindano la Nyimbo za Amani ambapo vikundi 19 kutoka Tanzania vitashiriki. Dhima ya tamasha la 12 ni Together as One: Amani ndio Mpango Mzima!

Busara Promotions, NGO inayoratibu tamasha la Sauti za Busara, ingependa kuchukua nafasi hii kutoa ukumbusho kwamba vyombo vya habari vyenye pasi za tamasha kwa waandishi ndio watakaopata ruhusa ya kuingia katika tamasha na kupata nafasi ya kuhudhuria press conferences, mikutano yote na waandishi wa habari, chumba chenye wi-fi katika eneo la tamasha, mahojiano na wasanii wa tamasha pamoja na majadiliano ya Movers & Shakers.

Kwa waandishi wenye kamera, pasi/vibali vitakuwezesha kupata eneo la mbele la wapiga picha (karibu kabisa na jukwaa) na kufanya shughuli ikiwemo kuweka visimamishi/tripod, visimamishi vya vipaza sauti, taa za ziada, au wafanyakazi zaidi ya mmoja.

Baadhi ya wafanyakazi wa tamasha na wasanii watakuwepo kujibu maswali na kukupa taarifa zinazoenda na wakati kuhusu tamasha la 12, katika Press Conference ya Dar es Salaam iliyopangwa kufanyika Alhamisi 29 Januari 2015, saa 3 asubuhi katika Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam.

0 comments:

 
Top