Sauti za Busara ni tamasha lililojipatia umaarufu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, ni tukio la kila mwaka ambalo limefanikiwa kuwekwa katika kalenda ya matamasha Afrika. Sauti za Busara huwaleta watu pamoja kusheherekea muziki wa Afrika bila ya kujali dini, rangi, tamaduni na wala wanapotoka. 

Busara Promotions inathamini na kushukuru Tanzania kama moja ya nchi zenye amani kuliko zote Duniani. Huku mwaka 2015 ukiwa ni mwaka wa uchaguzi Tanzania, taasisi hii isiyo ya kiserikali inaamini ili maendeleo yaendelee bila kizuizi, tunahitaji kuimarisha umoja, heshima katika utofauti na kufanya kazi ili kutunza na kulinda amani hii yenye thamani. Kama mwanamziki mwenye tuzo Baaba Maalkutoka Senegal anavyosema, ‘Njia kuelekea amani ya dunia inapatikana katika muziki na uwezo wake wa kuleta watu pamoja.’ 

Huku likiwaleta pamoja wasanii tofauti na watazamaji kusherekea muziki wa Kiafrika, Sauti za Busara inahodhi shindano, kukiwa na zawadi ya pesa taslimu ambayo ni pesa ya kurekodi kwa washindi wa Nyimbo za Amani. Mkurugenzi wa Tamasha, Yusuf Mahmoud anasema “Sauti za Busara 2015 litaisaidia kukuza amani kwa kutumia muziki; ambapo vikundi 15 kutoka Tanzania, sambamba na vingine vya Kimataifa vitatoa sauti za ujumbe wa amani, umoja na mshikamano katika maonesho yao. Tunatarajia kwamba (sauti) hizi zitasikika kwa nguvu na uwazi”

Wasanii wa Kitanzania katika shindano hili ni pamoja na Leo Mkanyia, Msafiri Zawose, Mohamed Ilyas, Zee Town Sojaz, Ifa Band, Mgodro Group, Mabantu Africa na wengine wengi. Shindano la Nyimbo za Amani linadhaminiwa na Busara Promotions, kwa msaada wa Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam. 

Shindano la Nyimbo za Amani litafanyika katika tamasha la Sauti za Busara Mji Mkongwe, Zanzibar kati ya saa 10:00 jioni siku ya Alhamisi tarehe 12 na saa 2:00 usiku siku ya Jumapili tarehe 15 Februari 2015. Shindano liko wazi kwa Wakazi wa Tanzania au Wazawa wa Tanzania. Vikundi vyote vya Kitanzania vinavyoshiriki kwenye tamasha vinaalikwa kutunga nyimbo maalum yenye dhima ya amani na umoja na kuifanyia onesho katika mida yao ya kutumbuiza katika tamasha. Fedha taslimu zitazawadiwa kwa ajili ya uzalishaji wa rekodi kitaalamu wa nyimbo zenye ubunifu: 4m/- TSh (Mshindi wa 1), 3m/- TSh (Mshindi wa 2) na 2m/- TSh (Mshindi wa 3)

0 comments:

 
Top