Mlezi Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi akiwa pia mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi ni jambo la kusikitisha kuona Uongozi wa Jimbo la Mtoni unashindwa kuliendeleza jengo la Kituo cha Afya cha Mtoni kutokana na itikadi za kisiasa.

Alisema jengo hilo lililoanzishwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya wananchi wa Viongozi waliopita wa Jimbo hilo kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu wa huduma za Afya wananchi wote wa jimbo la Mtoni.

Balozi Seif alisema hayo akiwa katika ziara ya siku mbili kukagua uhai wa chama cha mapinduzi katika Mkoa wa Magharibi akiwa mlezi ziara iliyompa fursa kukaguwa maendeleo ya matawi yaliyomo Wilaya ya Mfenesini pamoja na kuzindua Shina la UVCC Nambari moja la Tawila CCM Mwakaje.

Alisema wazo lililoanzishwa na viongozi na wananachi hao la kujenga kituo hicho linafaa kuungwa mkono kwa vile wananachi watakaopata huduma za afya baada ya kukamilika kwake hawategemei itikadi yoyote ile ya kisiasa.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaahidi wana CCM hao pamoja na wananachi wa Mtoni sambamba na Wilaya ya Mfenesini kwamba Serikali itaimaliza Hospitali hiyo ili lengo lililokusudiwa na wananachi hao linanze kutekelezwa mara moja.

Alifahamisha kwamba atashauriana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein kuona namna Serikali itakavyoongeza nguvu katika kuona jengo hilo linakamilika kama llivyopangwa.

Akigusia suala la kisiasa Balozi Seif aliwatahadharisha vijana kuwa makini na makundi ya watu wanaotumia vipindi vinavyokaribia wakati wa uchaguzi kuwatumia vijana katika kuwagawa wanachama wa chama hicho.

Alisema Vijana ni vyema wakaelewa kwamba wao ndio muhimili wa chama katika kukiongezea nguvu za kuendelea kushinda changuzi zote na akawapongeza Vijana wa Shina nambari moja la Mwakaje kwa uamuzi wao wa kuanzisha shina hilo.

Alieleza kwamba chama cha Mapinduzi kinaamini kwamba uanzishwaji wa mashina ya chama katika matawi mbali mbali hapa nchini ndio njia kuu ya kuu ya kuimarisha nguvu na uhai wa chama chenyewe.

Mlezi huyo wa Mkoa wa Maghribi aliwakumbusha Viongozi wa Matawi na Majimbo la Mkoa huo kuendelea kuwahamasisha wanachama wao kulipa ada za uanachama pamoja na kufanya vikao vya chama ili kuondosha wanachama magarasa.

Alifahamisha kwamba Tawi au Jimbo lisilofanya vikao vyake kama kawaida kwa mujibu wa kalenda ya chama cha Mapinduzi ni kukaribisha fitna na majungu ambayo hatimae husababisha mgawanyiko na kuleta makundi ndani ya chama.

Aliwaeleza wanachama hao wa CCM na Wananchi wa Wilaya ya Mfenesini kwamba CCM ndio yenye dhamana ya kulinda na kusimamia amani na utulivu kwa wakati huu nchini Tanzania.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi aliwapongeza Viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Mfenesini kwa juhudi zao za kutekeleza nsera na ilani ya Chama.

Akizungumzia suala la Katiba Mpya iliyopendekezwa na bunge Maalum la Katiba Balozi Seif aliwashauri Wananchi hasa Vijana kuendelea kuhamasishana katika dhana nzima ya kujiandaa kuipigia kura katiba hiyo wakati wa kura ya maoni.

Alisema Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum imekidhi mahitaji kamili ya kila kundi jambo ambalo inaonyesha kuungwa mkono pia na baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani hapa nchini.

Katika kuunga mkono juhudi za wanachama hao wa CCM Balozi Seif ameahidi kusaidia ukamilishaji wa mlango wa Duka la Shina ya Umoja wa Vijana wa CCM nambari moja la Tawi la Mwakaje.

Katika risala na taarifa zao tofauti wana CCM Hao wa Matawi yaliyomo ndani ya Wilaya ya Mfenesini Kichama wamelipongeza Bunge Maalum la Katiba kwa uwamuzi wao wa kupendekeza Katiba inayokubalika na wananachi walio wengi Nchini Tanzania.

Walisema Katiba hiyo imeweka wazi haki na maslahi ya kila kundi wakiwemo walemavu, vijana watoto na wanawake.

Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf alisema Uongozi wa CCM Mkoa huo umejipanga vyema tayari ukijianda na maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Mlezi huyo wa Mkoa wa Magharibi Balozi Seif Ali Iddi mapema asubuhi alizindua shina nambari moja la Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la CCM Mwakaje, kutembelea Matawi ya CCM Sharifumsa, Mtoni pamoja na Kukikagua Kituo cha Afya kinachojengwa pembezoni mwa Msuli ya Msingi ya Mtoni.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top