Wananchi wanane kati ya kumi (80%) wanafikiri kuwa Tanzania inapaswa kubakia ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Aidha, wananchi tisa kati ya kumi (85%) wanakubali uwepo wa ushirikiano mkubwa zaidi na Kenya naUganda. Wananchi sita kati ya kumi pia wanauunga mkono upanuzi wa ushirikiano na Rwanda (62%) pamoja na Burundi (59%).
Matokeo haya yalitolewa na Twaweza ikishirikiana na Society for International Development (SID) katika utafiti wenye jina la Hima tujenge nyumba moja! Watanzania wana maoni gani kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki. Msingi wa muhtasari huu ni takwimu kutokaSauti za Wananchi, utafiti wa kwanza wenye uwakilishi wa kitaifa barani Afrika unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi uliohoji washiriki kutoka kaya mbali mbali Tanzania Bara. Takwimu zilikusanywa Agosti 2014.
Mbali na kuunga mkono ushirikiano huu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wananchi kwa ujumla wanaamini athari zake zitakuwa chanya. Kipengele kilichoaminika kuliko vyote ni kile cha uchumi; wananchi mara mbili kwa wingi wanafikiri kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na athari chanya kiuchumi (42%), ikilinganishwa na wanaofikiri italeta athari hasi (20%). Vile vile, wananchi wengi wanafikiri Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na athari chanya badala ya hasi katika usalama (37% dhidi ya 20%), siasa (35% dhidi ya 25%) na utamaduni (33% dhidi ya 24%).
Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, vichwa vya habari kuhusu ushirikiano huu viliweka msisitizo kwenye uundwaji wakinachojulikana kama: “Umoja wa Hiari”. Hili ni kundi la wanachama waliojiunga nakukubaliana kuongezwa kwa kasi ya mchakato wa ushirikiano. Ni mtu 1 tu kati ya watu 5 (20%) aliyewahi kusikia kuhusu Umoja huo na kati yao, asilimia 67% wanafikiri kuwa Tanzaniainapaswa kuwa sehemu ya Umoja huu. Katika kundi la wale waliokuwa hawafahamu kuhusu Umoja huu, majibu yao yalikuwa yamegawanyika; 40% walipenda Tanzania ijiunge na 43% walipinga swala hilo.
Ingawa wananchi wanaonekana kwa kiasi kikubwa kuipendelea Jumuiya ya Afrika Mashariki na ushirikiano mkubwa zaidi kwa ngazi ya dhana; matokeo ya kuvutia zaidi yalijitokeza walipoulizwa kutoa mapendekezo mahususi. Msimamo wao ulikuwa dhahiri. Zaidi ya nusu ya wananchi wanakubali mapendekezo yafuatayo:
· Visa ya pekee ya utalii kwa kanda (82% wamekubali)
· Uwezo wa kusafiri katika kanda kwa kitambulisho cha taifa (82% wamekubali)
· Miradi ya pamoja ya miundombinu (78% wamekubali)
· Uhuru wa raia kufanya kazi popote ndani ya nchi wanachama (69% wamekubali)
· Pasi ya kusafiria moja (67% wamekubali)
· Biashara huru (bila kodi) (58% wamekubali)
· Sarafu moja (55% wamekubali)
Mapendekezo pekee ambayo hayakukubaliwa kwa wingi (kishindo) ni kuundwa kwa jeshi la pamoja (64% wamekataa), uhuru wa kumiliki ardhi (70% wamekataa) na Serikali moja yenye Bunge moja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (71% wamekataa).
Kwa kuangalia mustakabali, Watanzania wanayo matumaini kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa ni sehemu muhimu ya maisha yao. Washiriki 4 kati ya 10 (42%) wanasema kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa imara na Tanzania itakuwa mwanachamamuhimu. Hata hivyo, ni mtu 1 tu kati ya watu 10 (12%) anayefikiri kuwa biashara na Jumuiya ya Afrika Mashariki ni fursa muhimu kwa nchi yetu. Lengo kwa ajili ya baadaye ni utalii na uchimbaji madini ambayo wananchi 6 kati ya 10 (57%) wanafikiri inatoa fursamuhimu zaidi kwa Tanzania ya siku zijazo.
Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mwandamizi wa Society for International Development alitoa maoni yafuatayo kuhusu utafiti huu: "Matokeo haya yanatulazimisha tubadilishe mawazo yetu juu ya ushirikiano wa kikanda. Watanzania wanaunga mkono nchi ya Tanzania kushiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia wametaja mapendekezo yao pamoja na matumaini yao juu ya maisha yetu ya baadaye ndani yaJumuiya ya Afrika Mashariki. Maoni haya ni tofauti kabisa na simulizi za kuwa Watanzania wanapinga au ni waoga wa ushirikiano mkubwa wa kanda au kwamba wana wasiwasi kuhusu nchi fulani kupata faida kubwa kutokana na kufungua mipaka kwa ajili ya bidhaa, huduma za kazi au fedha."
Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, aliongeza: "Wananchi wamenena, maoni yao yakionyesha dhahiri kauli moja: wanaunga mkono nawana matumaini kuhusu ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kazi iliyopo kwa watunga sera wetu ni kuhakikisha kuwa tunaheshimu mahitaji haya na kuhakikisha kuwa Tanzania inashika nafasi thabiti ili kufaidika na fursa zitakazotokana na ushirikiano
0 comments:
Post a Comment