Msajili wa Vyama vya Siasa Nchni Tanzania ameombwa kuliangalia kwa umakini kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Watanzania { UKAWA } lilioamua kuenesha mikutano ya hadhara inayoashiria mfumo wa kisiasa bila ya kuzingatia taratibu za kisheria zinazofuata usajili rasmi.


Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi wakati akisalimia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kiband Maiti Mjini Zanzibar.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kundi hilo lililoundwa na baadhi ya Viongozi wa juu wa vyama vyasKisiasa vya Upinzani limeshindwa kutekeleza kazi waliyotumwa na Wananchi ya kutengeneza mfumo wa kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalum la Katiba.

Alisema kitendo cha Viongozi hao ambacho kinawakosesha wananchi lile wanalolihitaji kinafaa kiangaliwe kwa umakini na msajili wa vyama vya siasa kwa vile kinaweza kuwakosesha wananchi hao muda wao wa kushughulikia mahitaji yao ya Kimaendeleo na kujikita zaidi katika mikutano hiyo yenye ushawishi zaidi wa kisiasa.

Balozi vSeif aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kujiepusha na kundi hilo ambalo limekuwa likichukuwa kodi zao bila ya kutekeleza majukumu waliyo wakabidhi.

“ Kama kweli wana uchungu na nyinyi wananchi mbona walisubiri kwanza kutia mfukoni mkwanja { posho } halafu ndio wakaingia mitini kuvikimbia vikao vya Bunge Maalum kwa kujenga hoja “. Alisema Balozi Seif.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwaonya wale viongozi wa siasa wenye tabia ya kumsakama katika majukwaa ya kisiasa kuachana na tabia hiyo mara moja kwa vile wengi kati yao anawaelewa udhaifu wao wa Kisiasa.

Alisema endapo kama viongoz hao wataendelea na hulka hiyo waelewe kwamba muda si mrefu atalazimika kufichua maovu na aibu zao.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top