Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania ambae pia ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia Muungano Mh.Samia Suluhu Hassan Kushoto akiwa pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi katika Tafrija ndogo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo mara baada ya kuchanguliwa kuliongoza Bunge hilo linaloendelea kukutana Mjini Dodoma
Washiriki wa Tafija fupi ya Kupongezwa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samule Sita na Makamu wake Mh. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Mkahawa wa China uliomo ndani ya Dodoma Hoteli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mh. Moh’d Aboud Moh’d akifanya mzaha kunogesha tafrija ya kupongezwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Kulia ya Waziri Aboud ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar Mh. Salum Turky, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samuel Sita pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samuel Sita akitoa neno la shukrani mara baada ya Tafrija fupi ya kupongezwa kwake yeye na Makamu wake Mh. Samia Suluhu hapo Chinese Restaurant Mjini Dodoma.


0 comments:

 
Top