Baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya Uzi na N’gambwa  wadogo kwa wakubwa wakiendelea na harakati za matengenezo ya Bara bara yao itokayo Unguja Ukuu hadi Uzi kila baada ya kupuyngua kwa kina cha maji.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Bara bara ya Unguja     Ukuu – Uzi Bwana Shaya Mohd akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif eneo lenye kupitisha maji mwengi ambayo huleta kadhia kwenye Bara bara yao.
 Balozi Seif akikagua kwa kina Bara bara ya Unguja Ukuu hadi Uzi ambayo iko katika kiwango cha mawe ambacho kimesimamiwa na Wananachi wenyewe
 Moja ya Visima vichache vilivyomo ndani ya Kijiji cha N’gambwa ambavyo vina upungufu mkubwa wa maji kiasi kinachochangia kuleta usumbufu wa huduma hiyo ndani ya Kijiji hicho.
  Mzee Khatib Mussa wa Kijiji cha N’gambwa akimlalamikia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kadhiaya muda mrefu  inayowasumbua ya ukosefu wa huduma za Maji safi na salama kijijini pao.
 
 Katibu wa Kikindi cha Ushirika cha Hapa Kazi chenye wanachama 48 katika Kijiji cha Uzi ambae ni Mlemavu Bibi Mwanajuma Harufu Haji akimnon’oneza Kitu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kuzungumza na wananachi wa Vijiji vya Uzi na N’gambwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika Picha ya Pamoja na wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Uzi mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Uzi na N’gambwa.

0 comments:

 
Top