Sauti za Busara (Sounds of Wisdom) tamasha linalojulikana kama ‘Tamasha rafiki katika Sayari’ ni tamasha la kimataifa linalosheherekea muziki wa kiafrika kila mwaka wiki ya pili ya mwezi wa Februari.

Lengo likiwa ni kuwaleta watu pamoja na kuonyesha utajiri wa muziki wa kisasa ambao umebuniwa katika nchi za Afrika Mashariki, nchi nyingine kutoka barani Afrika na kwingineko duniani.

 Mwaka huu tamasha la 11 la Sauti za Busara litafanyika kuanzia tarehe 13-16 Februari katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe, Zanzibar. Jumla ya vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100% live. Vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19. Zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki, wasa nii hao wanatoka Afrika Mashariki, Afrika Kusini na Magharibi, maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico!

Miongoni mwa sanaii maarufu kutoka Tanzania watakaoshiriki tamasha la Saut i za Busara 2014 ni Jhikoman, mwanamuziki anayejulikana kwa muziki wake wa reggae ambae atazindua ziara yake ya kuitembelea dunia jukwaani wakati wa onyesho lake katika tamasha la Sauti za Busara! Wasanii wengine kutoka Tanzania watakashiriki tamasha ni Ashimba, Swahili Vibes, Hoko Roro, Seven Survivor, Abantu Mandingo, Segere Original, na Kazimoto, anayemshirikisha Jackie Kazimoto kutoka the internationally-acclaimed Jagwa Music.

 Busara pia itamkaribisha mwanamuziki mkongwe aliyefanikiwa kimuziki kutoka nchini Ghana Ebo Taylor, pia atakuwepo Sona Jobarteh mwanamke mwanahistoria kutoka nchini Gambia, na Jupiter and Okwess International mwanamuziki mwenye mafanikio kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo ambae anapasua anga katika fani ya muziki Afrika na kwingineko duniani. 

Kwa upande mwingine mwaka huu, burudani ya muziki itajumisha paredi siku ya ufunguzi, pia kutakuwa na Movers & Shakers (kongamano la watalamu), n a uonyeshaji wa filamu ndefu za muzki za kiafrika ambazo zimeshinda tunzo mbalimbali.
 
Kwa kushirikiana na wafadhili wa miradi HIVOS, Pia tutautambulisha mradi mpya unaojulikana kama “Santuri Safari”, mradi ambao utaangalia zaidi jukumu la DJ kwa wakati huu na kuangali jinsi ya utamaduni wa DJ katika kukuza muziki wa Afrika Mashariki. DJ waalikwa, wazalishaji wa muziki, wataalamu wa sauti, waandaji wa matamasha na wataalamu wa sanaa kutoka ukanda wa Afrika watajumuika pamoja Zanzibar na kufanya kazi pamoja na kupata mafunzo.
 
Tunaona hii ni fursa adhimu kushirikiana na kuangalia kuibuka kwa vitu vya kisasa vinavyotokea katika muzki wa electroniki na utamaduni wa MaDJ, na kuangalia jinsi ya kuukuza muziki kikanda na katika anga la kimataifa kwa wakati huu na kwa miaka ijayo. Kutakuwa na muziki kipindi cha jioni wakati wa jua kuzama (Sunset Sessions) maeneo ya mjini na siku ya ijumaa na jumamosi kutakuwa na burudani ya muziki (after parties) Ngome Kongwe baaya ya kumalizika kwa maonyesho ya moja kwa moja jukwaani (live).

 Wakati huo huo tamasha linakuza mambo mbalimbali kupitia “Buasara Xt ra” kwa kujumuisha matukio mbalilmbali ya maonyesho ambapo kwa pamoja hutoa fursa kwa wasanii wazawa kuonyesha kazi zao na kuwafanya wageni ; watembelea maeneo mengine ya kisiwa cha Zanzibar ambapo zaidi ya watanzania 150 huajiriwa kila mwaka kama wafanyakazi wa tamasha.
 
Kwa upande wa kukuza na kulinda muziki na utamaduni wa Zanzibar, Sauti za Busara inatumia nafasi iliyonayo katika kuuthamini muziki wa bara zima la Afrika, kukuza amani na kujenga jamii ya pamoja, kukuza utamaduni wa  Afrika Mashariki na kukuza utalii wa kitamaduni.

0 comments:

 
Top