Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu hatua ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuweka mikakati imara ya kukabiliana na matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini.

Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kuasi kikubwa kukabiliana na matatizo ya sekta hiyo yakiwemo upungufu wa vikalio na vitabu vya kusomea.

Mhe. Maalim Seif ameeleza hayo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la madarasa manane la skuli ya msingi Tumbe, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema tangu kufanyika kwa Mapinduzi hayo, Wizara ya Elimu imekuwa ikifanya juhudi za kuondosha matatizo hayo, lakini mikakati iliyopo sasa inaweza kumaliza matatizo hayo.

Aidha amewapongeza wananchi wa Tumbe na Micheweni kwa moyo wao wa kujitolea, pamoja na mwamko walionao katika kuchangia huduma za elimu.

Amesema kwa kipindi kirefu Wilaya ya Micheweni ilikuwa nyuma katika sekta sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, na kwamba mwamko unaoonyeshwa na wananchi hao umesababisha watoto wengi zaidi kupata fursa ya elimu.

Amewahimiza kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto ili kutunza maadili ambayo yanaonekana kuporomoka katika maeneo tofauti nchini, sambamba na kuwalinda dhidi ya marafiki waovu wanaoweza kuwatumbukiza katika vitendo viovu vikiwemo utumiaji wa wa dawa za kulevya.

Mapemba akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamhuna, amesema miongoni mwa mikakati yao ya kutatua kero za elimo ni pamoja kuanzisha miradi ya vitabu vya kusomea ambapo wanafunzi wote hadi darasa la nne watapatiwa vitabu vitano kila mmoja kuanzia mwezi Januari, 2014.

Amesema vitabu hivyo tayari vimeanza kukabidhiwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo Wilaya ya Micheweni.

Mkakati mwengine ni mdari wa kutengeza vikalio ambapo amesema tayari wamekusanya shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya utengenezaji wa vikali kwa skuli za Unguja na Pemba.

Kuhusu upungufu wa walimu wa sayansi, Mhe. Shamuhuna ameelezea ana matumaini kuwa tatizo hilo litamalizika karibuni kutoka na vyuo vikuu vya Zanzibar kutoa wahitimu wengi wa masomo ya sayansi kila mwaka.

Hassan Hamad (OMKR).

0 comments:

 
Top