Kwa kawaida neno mkimbizi sio geni kwenye midomo ya Watanzania na wenyeji wa mwambao waAfrika Mashariki, ingawaje mara nyingi neno hili hupewa watu wanaokimbia nchi zao kutokana na masuala mbali mbali ambayo hupeleka mtu mmoja au mwengine kukimbia kutoka katika eno lake. 

Lakini kiilivyo na hali halisi ilivyo kila mtu ni mhamiaji au ni kimbizi kwa njia moja au nyengine ila inatofautika kutoka na mazingira na matumizi ya maneno haya, ijakuwa kuwa kunatofauti kubwa kati ya MKIMBIZI na MHAMIAJI. 

Shirikia lisilo la kiserikali la International Organization of Migration (IOM) limeandaa mafunzo mafupi kwa waandishi wa habari kutoka Bara na Zanzibar kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao ili waweze kuwa na ufahamu juu ya suala zima mambo yahusuyo Ukimbizi na Uhamiaji hapa Tanzania. 

Ingawaje IOM inafanya kazi kwa karibu na shirika la UNHCR, lakini bado kunachangamoto kubwa ambayo mashirika haya yamekuwa yakikabiliana nayo na hasa katika maana na matumizi ya maneno hayo. 

Si vibaya tukisema kwamba kila mtu ni mkimbizi, ila kunahitajika kuwepo na sababu za kimsingi za kumfanya mtu Mkimbizi, ijapokuwa kila sabubu huwa ni ya msingi kwa mujibu wa mtu mwenyewe. 

Katika kuhakisha kwamba kila mtu anakuwa na uelewa sahihi juu ya dhana ya Ukimbizi na Uhamiaji mafunzo hayo ya siku tatu ambayo IOM imenza kuyatowa kwa waandishi wahabari kutoka kwenye vyombo mbali mbali itakuwa ni fursa adhimu na muhimu kwa Watanzania kuwefahamu kwa kina dhana hizo kupitia vyombo vya habari vya Tanzania na vile vya kimataifa kama vile BBC na DW. 

Kwa hakika katika muda huu mfupi ambao IOM imeweza kuwakutanisha waandishi wa habari ni jambo la maana na ni lamsingi sana katika kuhakika kwamba Watanzania wanaacha kuwa na mawazo potofu juu ya dhana ya Ukimbizi na Mhamiaji.

0 comments:

 
Top