Wananchi wa Micheweni wamehimizwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuitumia haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura wakati utakapofika.

Amesema mbali na upigaji kura katika uchgauzi mkuu wa mwaka 2015, uandikishaji huo pia ni muhimu katika kushiriki kura ya maoni ya kuamua juu ya hatma ya kupatikana kwa katiba mpya.

Akizungumza na wananchi baada ya kufungua Ofisi ya Jimbo la Tumbe katika Wilaya ya Micheweni, Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amewata wananchi kutopuuza fursa ya kujiandikisha ambayo tayari imeanza katika Wilaya hiyo.

Hivi karibuni Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ilitoa tathmini ya uandikishaji kwa upande wa Unguja, ambapo wananchi waliojitokeza ni chini ya asilimia 25.

Akizungumzia kuhusu Muungano, Maalim Seif amesema Muungano wa serikali mbili hauitendei haki Zanzibar.

Amesema kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa dola kamili iliyokuwa ikitambulika Kitaifa na Kimataifa, na kwamba wakati umefika kuirejeshea Zanzibar haki hiyo.

Hassan Hamad.

0 comments:

 
Top