Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amelithibitishia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba Barua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoziandika kuhusu ushiriki wake katika kutoa maoni ya mchakato wa rasimu ya mabadiliko ya Katiba mpya ya Tanzania ni sahihi. 

Balozi Seif ambae ni mbunge wa Munge hilo kutoka Jimbo la Kitope Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja alitoa kauli hiyo wakati alipoombwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo kusaidia ufafanuzi juu ya ushiriki wa Zanzibar kwenye mchakato huo ambao na tuhuma zilizotolew na upande wa upinzani ukidai kwamba Zanzibar haikushirikishwa katika suala hilo. 

Balozi Seif alilihakikishia Bunge hilo kwamba yeye ni mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya Rais wa Zanzibar kwa Mujibu wa Katiba ya Zanzibar hivyo alitahadharia hsakmba suala lolote linalotolewa na Mtu au kiongozi kupitia njia ya panya lisikubaliwe wala kupokelewa. 

Alisema Zanzibar kwa kiasi kikubwa imeshiriki vyema kwenye mchakato huo kwa kutumia taratibu zote zilizowekwa kupitia taasisi na jumuiya zote ambazo zilijitokeza katika mchakato huo muhimu kwa maslahi ya Taifa. 

Akitoa majumuisho hayo Waziri Chikawe, alisema serikali inalazimika kuendelea na mchakato huo, kwa vile sehemu kubwa ya hoja iliyokuwa ikibishaniwa ndani ya Bunge hilo haina nguvu kwa vile maandalizi ya mswada huo yaliweza kupata maoni kutoka Zanzibar. 

Alisema Wizara yake ilipokea maoni hayo kutoka kwa Waziri wa sheria wa Zanzibar kati ya mwezi wa tano ambapo inashangaza kuona Wajumbe wa CUF kuamuakutoa hoja za kutaka mjadala huo usiwepo wakati wakitambua Serikali ya Zanzibar hivi sasa imo katika mfumo wa umoja wa kitaifa na sio kama ilivyokuwa hapo awali. 

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo, alisema bado Wajumbe wa CUF walitakiwa kuona katika mjadala huo wanaisaidia serikali yao kwa kutambua ndani ya Bunge hilo wako kwa ajili ya kuisaidia na sio kuanzisha migomo jambo ambo linaweza kuikosesha Zanzibar kueleweka maoni yao. 

Alisema Wabunge wanapaswa kujua kuwa wao wapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi na ni vyema wakatumia nafasi zao kuhakikisha wanawawajibikia vyema. 

Alisema mswada huo una umuhimu mkubwa wa kuifanya kazi ya kuanzisha Bunge la Katiba kwa vile ndilo ambalo litaweza kuendeleza mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya hapo baadae. 

Alisema inafurahisha kuona msehemu kubwa ya mchakato huo katika ngazi mbali mbali zikiwemo za mijadala kwa wananchi na ndani ya mabaraza ambayo hivi sasa yanaendelea kufanya kazi zake vyema. 

Kutokana na hilo Waziri huyo, alisema ni vyema wajumbe hao kuona umuhimu wa kushiriki katika mchakato huo kwa amani ili kuifanya Tanzania kuwa na katiba nzuri ya hapo baadae. 

Nae Naibu Waziri wa Sheria Anjela Kairuki, akitoa maelezo yake alisema Tanzania ya kesho bado inahitaji kupata katiba nzuri itayoweza kuwafanya watanzania kuwa kiti kimoja. 

Akiahirisha Kikao cha Bunge hilo Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Piter Pinda amempongeza Mwandishi wa Habari anayejihusisha na uendeshaji wa Kipindi cha Maisha Plus Masoud Kipanya kwa mpango wake wa kuwajengea mazingira Vijana ya kuweza kujiajiri wenyewe. 

Mh. Pinda alisema mpango wa kuanzia miradi ya ufugaji nyuki inayosimamiwa na Mwandihi huyo inaweza kuisaidia Serikali kuu katika mapambano yake dhidi yha changa moto kubwa iliyopo ya ajira. 

Alimtaka Mwandishi huyo kuendelea na mfumo wa maisha endelevu badala ule ya kuigiza na kuwataka Watanzania wote kusaidia nguvu hizo katika kuona vijana wanajitegemea katika kuendeleza maisha yao kiuchumi. 

Akizungumzia suala la mchakato wa Katiba Waziri Mkuu Pinda amewapongeza Watanzania jitihada zao za kushiriki vyema katika mchakato huo ambao una lengo la kujenga hatma njema ya Taifa la Tanzania.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top