Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kuituza na kuindeleza miradi inayo fadhiliwa na Serikali zotembili na washirika wa maendeleo ili miradi hiyo indelee kuwanufaisha wananchi na kutimia lengo lililo kusudiwa.

Hayo ameyasema leo huko Jendele wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wakati alipo fanya ziara kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo ilio fadhiliwa na TASAF kupitia Serikali ya muungano Tanzania.


Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi kufadhili wana nchi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwalengo kwamba wananchi hao waweze kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato jambo ambalo baada ya mradihuo kukabidhiwa wananchi husuasua na hatimae kufa kituambacho hakifurahishi.


Amesema wana nchi wajifunze kuituza na kuendeleza miradi hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufahisha wao wenyewe.


“kuiacha miradi ife sivizuri ,muichangie iliijiwezekujiendesha na huko ndio faida ya miradi hiyo”.alisema Samia.


Aidha Waziri aliwambia wakulima wa bonde la jendele Kinyasini Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa hakuna sababu kwavile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo hivyo uzalishaji ungezeke.


Waziri hoyo alisema dhamira ya ziara yake kuja Zanzibar ni kuona vipi matumizi ya pesa za TASAF zinavyo tumika katika miradi ilio ombewa na utekelezaji wake umefikiaje kwa wananchi.


Waziri alifurahishwa na juhudi zinazo chukuliwa kwani kumefikiwa hatua kubwa za kumaendeleo na zinatia moyo kwa matumaini .


Waziri alitembelea mradi wa mpunga wa umwagiliaji maji jendele na mradi wa uzalishaji mbegu za mpunga kinyasini kisongoni na badae kupata maelezo juu ya miradi ASSP na SPDL inayo endeshwa na wizara yakilimo na maliasili na ushirika Zanzibar .


Miradi hiyo kwa TASAF ya awamu ya kwaza Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu ambapo ziligawiwa sawa sawa kwa unguja na pemba.


Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani 2,500.000.00 ambapo zilitumika kumalizia mradi wa kwaza unguja na pemba kupitia mifuko mitatu nayo ni mfuko wa Taifa wa kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs 2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya fedha TShs 1,800,000.000.00


Ziara hiyo itaendelea kasha kutembelea idara ya uhamiaji Zanzibar na malaka ya kitambulisha cha Taifa Zanzibar.


0 comments:

 
Top