Uelewa mdogo kwa wananchi juu ya suala zima la uhifadhi na usimamazi wa mazingira, imeelezwa kuwa ni moja ya changamoto ya usimamizi wa mazingira katika jiji la mwanza. Hayo yameelezwa leo na Afisa Mazingira wa mkoa mwa Bw. Charles Amani wakati akiota taarifa kwa naibu wazir Ofisi ya Makamu wa Rais katika Ziara ya kutembelea viwanda mjini Mwanza.

Pamoja na changamoto hiyo mkoa pia unakabilina na upungufu wa vifaa vya udhibiti wa taka ngumu na kutokuwepo kwa teknolojia ya ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira kwa hewa kutoka viwandani na kwenye magari pamoja na kutokuwa na dampo la kisasa.

Bw. Amani maeeleza kuwa pamoja na changamoto hizo, jiji la mwanza limekuwa likiongoza kwa usafi wa mazingira kwa kipindi cha miaka saba mfululizo, kutekelezaji wa kampeni ya upandaji miti pamoja na miradi mbali mbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Charles Kitwanga ameeleza kuwa lengo la ziara yake mkoani Mwanza si kufungia viwanda bali ni kutaka kuwa na msimamo wa pamoja na kuzingatia na kutekeleza sheria ya usimamizi wa mazingira, ili iwe yenye manufaa kwa watanzania, “lengo la kuja ni kuhakikisha sheria inafuatwa” alisisitiza.

Mh. Waziri aliongeza kwa kusema kusema kuwa ni vyema Halmashauri na wizara husika zikajipanga ili kuona namna ya kuwapatia sehemu mbadala wananchi wanaoishi milimani bila kuwabugudhi, ili kule nako kupangwe ili kuwe na mazingira endelevu.

Wakati huohuo, kamanda wa police wa kikosi maalum cha mazingira Nchini Bw. George Mayunga ameeleza kuwa jeshi la police lipo tayari kupambana na wahalifu wa mazingira,ili kujenga mazingira endelevu.

0 comments:

 
Top