Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Sazi Salula amewataka wadau wa sekta ya kilimo nchini hasa wakulima wadogo wadogo kujitahidi kufahamu athari na changamoto mbalilmbali zinazoikabili sekta hii kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Alitoa rai hiyo wakati akifungua warsha ya siku mbili ya kitaifa ikihusisha wadau mbalimbali kuandaa mwongozo wa taarifa za kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za wakulima na wafugaji nchini.

Aliwaomba wajumbe wa warsha hiyo kutoa maoni yao ya kitaalamu ili kuhakikisha mwongozo unakuwa tayari kwa matumizi ya jamii za wakulima na wafugaji nchini mapema iwezekanavyo hasa ikinzingatiwa kuwa athari sasa zimeanza kuwa kubwa sana. Alisema mwongozo huu ni muendelezo wa juhudi za serikali katika kushughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi. "Juhudi hizi zitaiwezesha nchi kuhimili atahari za mabadiliko haya na kuchangia juhudi za kimataifa za kupunguza gesijoto" alisema Bwana Salula.


Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ufadhili wa Serikali ya Japana kupitia UNDP, kwa ajili ya kujadili mwomgozo huu wa kusaidia wakulima na wafugaji wadogo wadogo kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Washirki wa warsha hiyo ni kutoka kwenye taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Waziri mkuu, Wizara ya maji, Wizara ya habari na michezo, Wizara ya kilimo na baraza la Mazingira la Taifa(NEMC, Jumuia ya Wakulima Tanzanaia na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.


Madhumuni ya mwongozo huu ni kuwasaidia wakulima na wafugaji kuendeleza shughuli zao za ufugaji na ukulima katika maeneora ambayo yamebadilika kutokana na mabadiliko ya tabianchi.


Monica Sapanjo- Ofisi ya Makamu wa Rais

0 comments:

 
Top