Neno ubakaji kati upwa huu wa washali ni neon lenye maana pana kijamii na kisheria, ambapo jamii wanadhani kwamba matendo ya ubakaji ni miongoni mwa laana ambayo mtendaji hufanya hivyo kutegemea lengo lake.

Sehemu kubwa ya jamii ya Tanzania inaamini kwamba ubakaji umelezwa kwamba ni kumlazimisha mtu kufanya mapenzi bila ya hiari yake, na kumlazimisha huku ni kwa njia tofauti mfano kumlaghai kumpatia kazi, kumjengea nyumba, kumsomesha lakini pia hata kumdanganya mwanamke kumtaka kimapenzi kwa kisingizio cha kumuoa hili pia ni kosa na ni miongoni mwa njia kubwa na ubajaki nchni.

Kisheria ubakaji umetafsiriwa kwamba ni kufanya ngono na mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18, hata kama amekubali kwa hiyari yake lakini bado inabakia kuwa ni kosa kisheria.

Taarifa za ubakaji zipo nyingi na hasa vijijini, na zipo baadhi ambazo zimefikishwa mahkamani kwa ajili ya kuweza kupatiwa hukumu kulingana na kosa lenyewe, lakini zipo pia mabazo huishia kwa jamii kwa kulipana fidia na hatmae kesi hiyo humalizika kwa mtoto ambaye ameathiriwa na tatizo hili la ubakaji huhamishwa kijiji kimoja na kupelekwke kijiji kingine.

Kwa kawaida matendo hayo hufanya na watu wenye umri usiopungu miaka 30-55 ambapo mara nyingi hufanya bila ya kuwa na sababu za maana ila ni uhasidi ndio unaowasumbua akilini mwao.

Ipo baadhi ya mikoa ambayo imeathirika kwa matendo ya ubakaji ambayo husababishwa utumiaji nguvu kwa baadhi ya wanaume, ulevi, matumizi mabaya ya kipato, malezi, imani ya ushirikina, umaskini, wogo wa wazazi wa kike kwa waume zao, lakini pia taama ya kutaka mali ambayo mzee huamini kwamba kumuozesha mtoto wake mapema kunaweza kukabadilisha hali ya maisha yao ya nyumbani kiujumla, hii sio sahihi kwani inadumaza maendeleo ya mtoto wakike kiuchumi na kisaikolojia.

Aidha utamaduni na mila potofu juu wa uwezo na nafasi ya mwanamme katika jamii ndio inayoplelekea baadhi ya wanaume kuoa watoto wa shule, la lengo la kukidhi matanio yao ya kufanya mapenzi na washichana wadogo.

Nadhubutu kusema kwamba ubakaji ni tatizo la kitaifa na kimataifa, mbali na hayo, njia moja ya kuweza kulipunguza tatizo hili ni kufanya mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuzuia wanaume kuoa watoto wa kike walio chini ya miaka 18, ambapo kwa sasa sheria hii inamruhusu mwanamke aliye chini ya ungalizi wa wazazi wake kuweza kuolewa naaminisha kwamba yupo chini ya umri wa miaka 18.

Mpaka sasa kitu kikubwa cha kufanyiwa kazi ili kuhakisha kwamba ubakaji unaondoka au kupungua kwa sasa, ni kuhakikisha kwamba watuhumiwa na vitendo vya ubakaji wanafikishwa mahakamani na kuweza kuchukuwaliwa hatua zaidi za kisheria.

Inasikitisha kuona kwamba wengi wa waofanya matendo haya mabaya hushia mitaani bila ya kuchukuliwa hatua yoyote na wakati mwengine hudiriki hata kutoa vitisho kwa familia iliyoathirika na tatizo hili la aibu.

Si jambo la kushangaza kuona kwamba mtendaji wako akawa hana hatia na mtendewaji ndie akawa na hatia, kwa mfano mwanamke wa mwenye umri wa miaka 18 au zaidi ya hapo akifanyiwa ukatili huu wa ubakaji mara nyingi vidole hunyooshewa yeye na hutiwa hatiani kwa kuambi kosa ni lake kutokana na mazavi aliyovaa, lakini suala la kujiuliza mavazi na ubakaji kunauhusianao gani? Au ni ile njia ya kumtukaza mwanamme afanye atakalo?

Ikiwa kwa upande huu ni kosa la mtu mwenye lakini je kwa mtoto wa miako 5-10 kosa ni la nani baba?, mama?, dada au?.

Ninawasi wasi kwamba inawezekana pengine ipo misingi ya rushwa ambayo hupelekea mtuhumiwa asitiwe hatiani au ni ile misingi ya ujamaa, udugu na ujirani mwema ndio ambao hupeleka kesi hizi za upakaji zikawa zinaishia mitaani badaala ya mahakamani.

Njia pekee ya kuweza kuepukana na tatizo hili ni kuondosha muhali kwa mtuhumia ili haki iweze kuchukuwa mkondo wake, ni wajibu wa kila mzazi kuwa rafiki wa mtoto wake na sio adui wa mtoto wake na wa jirani yake, inawezekana timiza wajibu wako, ili kuiepusha jamii ya ubakaji pamoja na virusi vya ukimwi.

0 comments:

 
Top