Vijana nchini wametakiwa kuzitumia fursa
zilizowekwa na Serikali zote mbili katika sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi
ambazo tayari zimeonekana kuwanufaisha watu wengi waliojaribu waliojaribu
kufuatilia kwamakini.
Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni wakati akizindua sherehe
za Siku kuu ya Wakulima Nane nane mwaka 2012 katika Viwanja vya Maonyesho ya
Kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma.
Dr. Sheni katika Hotuba yake iliyosomwa kwa
niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema
ni muhimu kwa Vijana kutambua kuwa wana nafasi nzuri ya kuendeleza Maisha yao
na kutoa mchango mkubwa wa Maendeleo ya Taifa kwa kujishughulisha katika
Kilimo, Uvuvi na
Ufugaji.
Alisema inasikitisha kuona baadhi ya Vijana
wamekuwa na ndoto za kupata utajiri wa haraka ambao matokeo yake wanajiingiza
katika harakati zisizo na muelekeo zinazoishia kujitumbukia katika
vitendo viovu vinavyozorotesha jitihada za Taifa za kutafuta Maendeleo.
“
Dhana ya kuwa maisha bora yako mijini imeshapitwa na wakati. Mashambani
kunaweza kuwa na maisha bora zaidi kuliko mijini kwa sababu hakungojei mshahara
wa mwezi bali kuna mshahara wa kila siku”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Vijana wakati huu ni vyema
wakazingatia zaidi kuwa wao ndio nguzo kubwa ya Maendeleo ya Taifa lolote lenye
nia ya kuleta Maendeleo ya kudumu.
Alisema Sekta ya Kilimo bado inaendelea
kuwa mhimili wa Uchumi wa Taifa kwa
vile inatoa ajira ya zaidi ya asilimia 77.5% ambapo Wananchi waliowengi
wanaishi Vijijini.
Balozi Seif alifafanua kwamba Serikali
zote mbili zitaendelea kutekeleza mipango tofaui katika sekta hizo kwa
kushirikisha wananchi ili kuwawezesha na kuongeza kipato chao na hatimae waweze
kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa pato la Taifa.
Aliwahakikishia Wananchi kwama Serikali
zote zitajitahidi kuwajengea mazingira bora Wakulima, Wavuvi na Wafugaji
ya kumudu kununua bei za pembejeo, huduma za Matrekta kwa lengo la kupata
msukumo wa kuimarisha shughuli zao.
Alisisitiza kwamba mpango huo unalenga kwenda
sambamba na utoaji wa mafunzo na Elimu bora kwa wote watakaojishughulisha na
Sekta hizo za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Aliwakumbusha
Wananchi kuongeza bidii katika matumizi ya rasilimali ya Bahari, Maziwa, Mito
katika kuendeleza Sekta ya Uvuvi ambayo inasikitisha kuona kuwa mchango wa
sekta hiyo katika pato la Taifa ni asilimia 1.5% tu.
Balozi
Seif aliongeza kwamba Jamii inapaswa kuendelea kupiga vita vitendo yote
vya Uvuvi haramu ili kuifanya shughuli hiyo iwe ya kudumu na inayozingatia
mahitaji ya Jamii kwa sasa na hapo baadaye.
“ Ni
muhimu sasa kutunza mazingira yetu kuliko wakati mwengine wowote kutokana na
tatizo la tabia Nchi inayoikumba Dunia. Hatuna budi sote tuzingatie kauli
isemayo “ yatunze mazingira ili nawe yakutunze”. Alitilia mkazo zaidi Balozi
Seif Ali Iddi.
Aliwapongeza waandaaji wa maonyesho hayo ya
nane nane kwa jitihada zao zilizopelekea kufanikisha maandalizi yanayoridhisha
na kuwaomba Wananchi kuhudhuria kwa wingi ili kujifunza mbinu bora na za Kisasa
za uzalishaji katika sekta za Kilimo, Ufugaji na
Uvuvi.
“ Nimefurahi kuona kuwa Wakulima, Wavuvi na
Wafugaji kutoka Mikoa yote ya Tanzania wako hapa kwa ajili ya kujifunza na
kusherehekea sherehe hizi. Shrehe zimefana sana.Hongereni sana”. Balozi Seif
alikuwa akimwaga sifa kem kem.
Akitoa
Salamu za Wakulima Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania {TASO
} Bwana Angrei Moyo aliimba Serikali kuandaa sera Maalum kwa wote ya uendehaji
wa sherehe za nane nane kwa lengo la kuondoa matatizo ya mawasiliano katika
ushiriki wa wadau wa Sekta hiyo.
Bwana
Moyo utekelezaji wa pamoja ktika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa Taifa zinaweza
kuleta tija kwa faida ya Jamii yote ya Watanzania hasa Wakulima, Wavuvi na
afugaji.
Mwenyekiti huyo wa Chama cha Wakulima
Tanzania pia alisisitiza umuhimu wa Teknolojia ulenge zaidi kwa wadau hao ili
kuimariha mbinu za Kisasa za Uzalishaji.
Akimkaribisha Mgei rasmi katika uzinduzi wa
Sherehe hizo za wakulima nane nane Naibu Waziri wa Kilimo na Ushurika Mh.
Adam Malima ameyashukuru mashirika yote ndani na nje ya Nchini kwa juhudi zao
za kusaidia Sekta ya Kilimo ambayo ndio mama kwa Uchumi wa Taifa.
Mh. Malima alisema uungaji wao
mkono umepelekea kuongeza kasi ya uzalishaji hasa kwa wakulima wa kipato cha
chini vijijini ambao wanafkia asilimia 77.5% ya watu wote Nchini
Tanzania.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua mradi mkubwa wa shamba
la Mizabibu katika Wilaya ya Chamwino unaoshirikisha Wakulima wa eneo hilo
katika mpango wa ukulima wa bega kwa bega.
Balozi Seif amepongeza hatua za
kuanzishwa kwa maradi huo ambao ni mfano kwa vile umeanzishwa na Wakulima
wenyewe jambo ambalo linafaa kuigwa na Sekta nyengine za uzalishaji
nchini.
Alisema
uwezo wa Wananchi wa kujiajiri wenyewe uo endapo Wataalamu watawaandalia
miundo mbinu boraitakayokidhi mahitaji yao sambamba na uwezeshwaji
kifedha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif pia alipata fursa y kutembelea mabanda mbali mbali ya ualishaji wa
Washirika hao wa sekta ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kutoka mikoa mbali mbali
Nchini Tanzania.
Ujumbe wa mwaka huu wa maadhimisho ya sherehe za nane nane unasema Kilmo kwanza
zalisha Kisayansi na Teknolojia kukidhi mahitaji ya idadi ya Watu Nchini .
Othman KhamisAme
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
0 comments:
Post a Comment