Chebli Masaidie
Tamasha la Sauti za Busara ambalo lilianza February 8,2012 lilifikia ukingoni jana baadaya ya wasanii kutoka walipoweza kulishambulia jukwa la sauti za busara huku Chebli Masaidie, akizikonga nyoyo mashabiki wake katika ukumbi wa Mambo Clab, Ngome Kongwe.
ingawaje ngoma nyingi za  asili ziliweza kupingwa kama mdundiko, ngongoti, dufu na shangwe katika maandamano maarufu kama Carnival Parade ambayo yalianzia Kisonge Park saa kumi kamili jioni na kuishia Ngome Kongwe saa kumi na mbili jioni lakini bado ipoa haja ya kuweza kutafuta njia bora za kuweza kulifanya tamsha hili kuwa bora zaidi.
Mbali ya kuwepo kwa vikundi vingi ambavyo vimeweza kuwaburudisha wananchi wa Zanzibar, kikiwemo kikundi cha Mkota Spirit Dancers kutoka Pemba, Swahili Vibes, Shirikisho Sanaa, Tandaa Traditional Group, Wanafunzi wa SOS, Ary Morais (Cape Verde/Norway) na Mashauzi Classic modern taarab ya Tanzania ikiongozwa na Isha Mashauzi, lakini bado wasanii wengine wamekuwa wakiachwa mkono kutokana na uwezo wa wasanii wenyewe au afisi za busara kutokuwapa kipau mbele wasaanii hao.
kwa kiasi kikubwa wasanii wa Zenj Flava wamekuwa wakikosekana jukwaani, bila ya kuwepo kwa sababu maalumu, inawekena kabisa pengine ni gharama za kuwalipa au uwezo mdogo wa wasanii wa Zanzibar au? kwa kweli hatujuwi lakini iwe iwavyo tamasha hili lipo kwa ajili ya kulinda na kutunza tamaduni za watu wa Zanzibar, iwaje wasaanii wa visiwa hivi hawapati nafasi ya kushiriki katika tamashi hili muhimu?
Ni ukweli suiofichika kwamba kikundi kilichotoka Pemba, Mkota Spirit Dancers kilifanya onyesho zuri  iliyopambwa na mavazi na nyimbo za  kiasili ambapo nyimbo kama zile za  ‘Uganga Ukuu’, ‘Ng’ombe alia Baa’, ‘Ukaruka Mgongowa’ na ‘Bamba la Mvumo' kwa kiasi kikubwa ziliwakuna mashabiki wa muziki wa asili wa zisiwa hivi.
Mbali ya kuwepo kwa vikundi na ngama mbali mbali lakini ipo haja kwa waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara kuwafikiria zaidi jinsi ya kuwasaidia na kuwainua wasaani wa Zenj Flava, kwani kushiriki kwao katika tamasha ndio njia pekee ya kuweza kuitangaza Zanzibar na tamasha kwa ujumla.

0 comments:

 
Top