Kikao cha Kamati ya pamoja ya  Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya   Mapinduzi ya Zanzibar kimekutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal.
Kikao hicho kilichohusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, Watendaji wa Serikali wakiwemo pia  Wataalamu kilifanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza Mjini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kikao hicho walikubaliana kuthibitisha kumbu kumbu za Kikao cha Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ cha Tarehe 2 Juni mwaka 2010 kilichokutana Bwawani Mjini Zanzibar.
Halkadhalika Wajumbe hao walipitia Taarifa ya Utekelezaji  wa yatokanayo na Kikao hicho ambayo ni Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta  na Gesi asilia, Uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu na Ushirikiano wa Zanzibar na Taasisi za Nje.
Taarifa nyengine  ni ajira kwa Watumishi wa Zanzibar katika Taasisi za Muungano, mgawanyo wa Mapato yatokanayo na faida  ya Benki Kuu, Malalamiko ya Wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili walingizapo bidhaa zao Tanzania Bara, usajili wa vyombo vya moto,    likiwemo pia ongezeko la gharama za umeme kutoka Tanesco kwenda ZECO na Uharamiawa  na utekaji nyra meli.
Katika Majadiliano hayo Mwenyekiti wa Kikao hicho Dr. Mohd Gharib Bilal aliagiza mamlaka zinazohusika kutoa maelekezo ndani ya kipindi cha miezi mine kuhusu suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta  na Gesi asilia.
Mapema Mwanasheria Mkuu waSerikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman alisema taratibu zote na Baraka kuhusu suala hilo zimeshachukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi na kuliwasilisha Serikali ya Muungano kwa hatua za kisheria.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi alisisitiza haja ya kuwa na  ratiba maalum ya vikao pamoja na kupunguza urasimu wa utekelezaji wa maamuzi yanayofikiwa katika vikao hivyo vya pamoja.
Balozi Seif alisema hatua hiyo itapunguza kero zilizopo na hatiae kuamsha ari ya kuimarisha Muungano kwa pande zote mbili.
“ Nirahisishieni kazi ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa wajumbe wake wako Solidarity na hakuna Mjumbe wa CCM wana CUF katika suala lolote linalohusu Muuungano ”. Alisisitiza Balozi Seif.
Katika kikao hicho upande wa Wajumbe wa Serikali ya Muungano uliongozwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda wakati ule wa Zanzibar Uliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba

0 comments:

 
Top