Novemba 17, 2011, Busara Promotions itakutana na wadau kutoka sekta ya utalii ya Zanzibar pamoja na maafisa kutoka serikalini kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuiendeleza kisiwa cha Zanzibar kwa kupitia tamasha la muziki, Sauti za Busara. Kikao hiki kitawakutanisha mawakilishi kutoka sekta za umma na za binafsi kuchunguza matokeo ya matamasha ya Zanzibar, kuimarisha uhusiano na kuendeleza miungano ya kikazi.
“Tamasha hili linaimarisha uchumi wa ndani. Mahoteli yalioko ndani na nje ya Stone Town yanapata wageni wengi kipindi cha tamasha na hata nafasi za ndege na tiketi za vifuko kukosekana; madereva wa mateksi wanapata biashara na maduka yanajaa wateja. Sauti ya Busara ilipoanzishwa, mwezi Februari ilikuwa kipindi cha biashara ndogo kitalii. Leo hii, mwezi Februari imekuwa kipindi mojawapo cha biashara nzuri zaidi, ahsante kwa tamasha hili. Takwimu za Tume la Utalii Zanzibar zinaonyesha kuwa watalii wanaofikia Zanzibar mwezi Februari ya kila mwaka wameongezeka maradufu kwa asilimia 400 tangu kuanzishwa kwa tamasha hii.” alisema Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi wa Busara Promotions. Licha ya ongezeko ya watalii pamoja na mapato, uendeshaji wa tamasha la Sauti za Busara bado linatuwia ugumu kwenye kupata ufadhili. Kipindi cha tamasha, kiingilio huwa ni bure kabla ya machweo, na pia huwa ni bei ndogo kuwawezesha Wazanzibari wote kujumuika kwenye tamasha.
“Tusipoungwa mkono na Serikali pamoja na wafanyabishara wa ndani, hatutaweza kuiendeleza tamasha la Sauti za Busara Zanzibar baada ya mwaka 2012.” alisema Yusuf Mahmoud ambaye ameisimamia tamasha kwa ufanisi kutoka mwaka 2003.
Wakati wahisani wengi wakitarajia mashirika ya sanaa kuweza kujitegemea kwa kupitia miungano ya umma na binafsi, wadau wa ndani bado hawajaona umuhimu wa kuyaunga mkono matamasha ya kitamaduni kama Sauti za Busara. Nia ya mkutano huu ni kuweza kuwajulisha wadau watarajiwa kuhusu njia mbali mbali za kuweza kuiunga mkono tamasha la Sauti za Busara, kuanzisha mazungumzo na kuleta ufahamu kuhusu tamasha.
Huu mkutano umepangwa kufanyika tarehe 17 mwezi Novemba mwaka huu, ikiwa ni siku ya Alhamisi, kwenye hoteli ya Zanzibar Beach Resort kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

0 comments:

 
Top