TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI

Ndugu wanachama Zanzibar Press Club.
Uongozi wa ZPC unafuraha kuwatangazia wanachama wote wa ZPC kwamba ifikapo tarehe 23.10.2011, ambapo itakuwa siku ya Jumapili kutakuwa na MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI ambao utaambatana na marekebisho ya KATIBA YETU.
Hivyo basi, UONGOZI unawatangazia wanachama wake wote kushiriki katika uchaguzi huo kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya wa kuiendesha KLABU. Ni vyema kila mwanachama ambaye anataka kugombea nafasi yoyote ya UONGOZI afike afisi za ZPC au awasiliane na Mwenyekiti wa ZPC Nd.Enzi Talib Aboud kwa simu namba 0777 434893 au Katibu Mtendaji Nd.Ali Bakari Othman kwa simu namba 0777 422061 au paruapeperushi zanpress@yahoo.co.uk au zanpress@hotmaill.com kwa ajili ya kuja kuchukuwa fomu. Nafasi zinazogombewa ni:-
1. Mwenyekiti
2. Katibu Mtendaji
3. Naibu Katibu Mtendaji
4. Mhasibu
5. Pamoja na Wajumbe sita (6) wenye uwiano sawa wa kijinsia
Ni vyema kila mwanachama kuhakisha kwamba anasawazisha deni lake la uanachama ili aweze kupata nafasi ya kushiriki ipasavyo katika uchaguzi huu, ikiwa ni pamoja na haki ya KUCHAGUWA na KUCHAGULIWA
Akhsant
Ali Bakari Othman
Katibu Mtendaji
ZPC

0 comments:

 
Top