Misaada ya Kiuchumi na maendeleo ya Ustawi wa Jamii inayoendelea kutolewa na Jamuhuri ya Watu wa China kwa Tanzania Tokea Uhuru inaashiria ushirikiano wa Kidugu uliopo kati ya Mataifa hayo mawili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seifa Ali Iddi ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Guan Club mwisho mwa ziara yake yakukagua miradi ya Maendeleo ya Kampuni ya Hongda Group ya Jimbo la Sichuan Nchini China.
Kampuni hiyo ndio mwenyeji wa ziara ya Balozi Seif Ali Iddi aliyeiwakilisha Tanzania kwa niaba ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda katika Tamasha la 12 la Maonyesho ya Biashara na Viwanda katika Jimbo la Sichuan Nchini China.
Balozi Seif alisema Watanzania wameshuhudia miradimbali mbali mikubwa iliyoekezwa na kuanzisha na China Nchini Tanzania Bara na Zanzibar mara baada ya Uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar.
Ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia { TAZARA }, Viwanda vya Sukari, Viatu, Sigara Zanzibar pamoja na Viwanja vya Michezo na Hospitali pane zote za Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Kampuni ya Hongda Group ya Jimbo la Sichuan kwa uamuzi wake wa kuingia ubia na Shirika la Maendeleo la Tanzania katika Mradi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Mchuchuma ulioko Wilaya ya Ludewa Tanzania Bara utakaogharimu jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni tatu .Balozi Seif amesema mradi huo ambao ni wa pili kwa ukubwa
Tanzania ukitanguliwa na ule wa Reli ya Tazara mbali ya kuongeza mapato kwa pande hizo mbili lakini pia utatoa ajira kwa kundi kubwa hasa la Vijana.
Alisema licha ya China haikuwa na Uchumi mkubwa katika miaka ya 60 na 70 lakini iliweza kuendeleza misaada yake kwa Tanzania na Zanzibar kwa jumla.
“ Kutoa ni moyo na wala si utajiri ndicho kitendo kilichofanywa na Ndugu zetu wa china katika kutusaidia ”. Alisema Balozi Seif .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameishauri Kampuni ya Hongda Group ya Jimbo la Sichuan kuendelea kuunga mkono maendeleo ya Tanzania hasa katika Sekta a UtaliiAmefahamisha kwamba mbali ya vivutio vizuri na Mali asili kadhaa zilizomo bali pia miundo mbinu imeshaimarishwa kwa kiwango cha kuridisha.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi yaKampuni ya Hongda Group Bwana Liu Canglong amesema uwekezaji wa China pamoja na Baadhi ya Makampuni ya Nchi hiyo Nchini Tanzania unatokana na Historia ndefu ya Pande hizo mbili,
Bwana Liu amesema ana imani kwamba Tanzania itapiga hatua za haraka za Maendeleo ikijizatiti na Kuiga mfano wa China.
Amesema mradi wa Mchuchuma ni mfano wa mabadiliko hayo yatakayotoa fursa ya ajira kwa Wana Vijiji watakaouzunguuka mradi huo.
Balozi Seif na Ujumbe wake anarejea Nyumbani Jumatatu jioni baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Kampuni ya Hongda Group katika Jimbo la Sichuani nchini China ikiambatana na kuhudhuria Tamasha la 12 la Maonyesho ya Biashar na Viwanda.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment