Wajumbe wa kamati ya kudumu ya mawasiliano na ujenzi ya Baraza la wawakilishi la Zanzibar walikutana katika kikiao cha dharura kilichofanyika leo tarahe 13-09-2011 katika ofisi za baraza la wawakilishi Zanzibar. Madhumuni ya kikao hicho ni kutafakari suala la maafa yaliyotokea siku ya tarehe 10-09-2011 kufuatia kuzama kwa meli ya MV. Spice Islander liyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba.
Kamati ya maasiliano na ujenzi kwa kauli moja inaunga mkono taarifa ya kamati ya Briefing ya Wajumbe wote wa Baraza la wawakilishi kuhusiana na maafa hayo ambayo ilitolewa kwa vyombo vya habari tarehe 12-09-2011. Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi kwa upande wake nayo inatoa mkono wa pale kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk.Ali Mohamed Shein, wafiwa wote na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kutokana na msiba huo mkubwa.
Kamati ya Mawsiliano na Ujenzi pia inaunga mkono na kupongeza juhudi zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, taasisi mbali mbali za Serikali na za watu binafsi, wananchi wote kwa ujumla bila ya kuwasahau ndugu zetu kutoka Afrika Kusini katika zoezi la uokozi na kutafuta miili ya watu waliofariki kutokana na ajali iliyotokana na meli hiyo.
Kamati inaomba juhudi hizo ziendelee ili tuweze kuokoa watu wengine waliofariki kutokana na ajali ambao bado miili yao haijapatikana.
Kutokana msiba huu mkubwa kugusa wananchi wengi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi inatoa wito kwa Serikali kuharakisha hatua za kufanya uchunguzi huo iweze kutolewa kwa wananchi haraka na hatua muafaka zitakazohitajika kuchukuliwa kutokana na ripoti hiyo, ziweze kuchukuliwa.
Mwisho. Kamati nayo inamuomba Mwenyezi-Mungu awajaalie wale wote waliookolewa katika ajali hiyo nguvu, afya njema, na umri mrefu na pia tumuombe Mwenyezi-Mungu awajaalie wenzetu waliofariki katika ajali hiyo makazi mema peponi, amin.
Mheshimiwa Makame Mshimba Mbarouk,Mwenyekiti,
Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi,
Baraza la Wawakilishi,
Zanzibar,
0 comments:
Post a Comment