Maiti tano zinazofikiriwa kuwemo kwenye meli ya m.v spice zimeokotwa katika ufukwe wa mombasa nchini Kenya. Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya maafa zanzibar Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi seif ali iddi ameeleza hayo afisini kwake vuga wakati akiendelea kupokea salamu za pole kutoka kwa wawakilishi wa taasisi na jumuiya mbali mbali waliofika fasini hapo kufariji.
Balozi seif amesema taarifa hizo zimekuja kufuatia mawasiliano kati ya serikali na Afisi ya ubalozi mdogo wa Tanzania uliopo mombasa nchini Kenya. Amesema maiti hizo tano zinafanya idadi ya maiti waliopatikana hadi sasa kufikia 202. Makamu wa pili wa rais amezishukuru taasisi zote zilizotoa mchango wao ambao unaashiriia kukugwa na msiba huo.
Balozi seif amesema taarifa hizo zimekuja kufuatia mawasiliano kati ya serikali na Afisi ya ubalozi mdogo wa Tanzania uliopo mombasa nchini Kenya. Amesema maiti hizo tano zinafanya idadi ya maiti waliopatikana hadi sasa kufikia 202. Makamu wa pili wa rais amezishukuru taasisi zote zilizotoa mchango wao ambao unaashiriia kukugwa na msiba huo.
Taasisi zilizowasilisha ubani wao ni pamoja na chama cha mapinduzi CCM makao makuu,wabunge wanawake wa bunge la afrika mashariki,jumuiya ya khoja shia isnashir ya afrika, uongozi wa baraza la wawakilishi Zanzibar,arusha wazee club, benki ya NMB kwa kusirikiana na baraza la manispaa Zanzibar pamoja na benki ya vitega uchumi Tanzania { TIB } pamoja na Kampuni ya IPP Media ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd amepokea michango kutoka taasisi tofauti zilizohamasika kuchangia familia zilizopatwa na maafa hayo. Waliochangia fimilia hizo ni pamoja na jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar{ zapha + }, Taasisi ya uwekezaji vitega uchumi Zanzibar { ZIPA }, Jumuiya ya Wanasheria Zanzibar { Zanzibar law Society }, Taasisi ya Huduma za Viwanja vya Ndege Tanzania { ceo }.
Akitoa shukrani zake Waziri Aboud amesema kwamba nia ya Serikali ni kuona kuendelea kuwatafuta watu wote ambao bado hawajapatikana kufuatia ajali hiyo. Wakitoa salamu zao za pole wawakilishi wa Taasisi hizo wameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuleta Heshima ya nchi kutokana na kukabiliana vyema na maafa hayo kwa Ushirikiano wao wa karibu na Wananchi na Taasisi za Uokozi. Jumla ya shilingi la Kitanzania milioni 148,200,000/- zimepokelewa kutoka kwa Taasisi na Jumuiya tofauti za ndani na nje ya nchi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment